Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNICEF/van Oorsouw

Jamii inaelewa nini kuhusu ukatili wa kijinsia

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women ukatili dhidi ya wanawake na wasichan unasalia kuwa kitendo cha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu duniani kote, ukiathiri zaidi ya wanawake milioni 1.3, takwimu ambayo hata hivyo haijabadilika kwa zaidi ya muongo mmoja

Sauti
3'46"
UN Women

Girl Shine ya UN Women imenijengea kujiamini na sasa nasaidia familia yangu- Rachael

Mizozo na umaskini wa kupindukia kwenye mazingira ya uhitaji mkubwa wa msaada wa kibinadamu huwaweka wasichana katika hatari kubwa ya kukumbwa na ukatili na kunyanyaswa. Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake, UN WOMEN kwa kutambua hilo linatekeleza miradi katika kambi za wakimbizi za Dadaab na Kakuma nchini Kenya ili kuwajengea uwezo wasichana barubaru ili hatimaye waweza kuandaa mustakabali bora wa maisha yao. Girls Shine ni moja ya miradi hiyo kupitia mradi mkubwa wa LEAP unaoungwa mkono na serikali ya Japan tangu mwaka 2018.

Sauti
3'13"
© Unsplash/Jose Chinchilla

Harakati za Benki ya Dunia kuuboresha mji wa Libiąż, Poland dhidi ya makaa ya mawe

Kuondoa makaa ya mawe ni mojawapo ya hatua muhimu zaidi za kupambana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda sayari. Kuhama kutoka katika matumizi ya makaa ya mawe hadi nishati safi hupatia jamii fursa muhimu za kiuchumi na kijamii pia. Mji wa Libiąż, Poland, ulio katika eneo la uchimbaji wa makaa ya mawe ambao umedumu kwa karne nyingi, uko katikati ya mabadiliko haya.

Sauti
3'27"
© UNICEF/Lamek Orina

Ukame Kenya: Serikali imeanza mchakato wa kufadhili Mfuko wa Taifa wa Dharura lakini tunahitaji usaidizi kuokoa maisha ya watu

Umoja wa Mataifa na wadau wake wa masuala ya kibinadamu nchini Kenya wameomba dola milioni 472.6 kusaidia watu milioni 4.3 walioathiriwa na ukame, ili kuunga mkono mwitikio unaoongozwa na Serikali, huku janga hilo likitarajiwa kuwa mbaya zaidi. Hali katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo katika Pembe ya Afrika, ni mbaya. Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua anaeleza kuwa mzigo huu wa janga la mabadiliko ya tabianchi ni mkubwa kwa nchi yake na kwa hivyo ni muhimu jumuiya ya kimataifa ikasaidia lengo hilo la Umoja wa Mataifa kwani hali ya wananchi inazidi kuwa mbaya.

Sauti
5'6"
FAO/Arete/Isak Amin.

Msaada kutoka FAO waleta matumaini kwa wakazi wa Hirshabelle nchini Somalia

Ukame wa zaidi ya miongo minne na mafuriko vimekuwa ‘mwiba’ kwa wananchi wa Somalia na hivyo kutishia uhakika wa kupata chakula halikadhalika mbinu za kujipatia kipato. Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO kwa msaada kutoka serikali ya Sweden imewezesha mradi wa kusaidia wakulima wadogo kwa kuwapatia pembejeo na msaada wa fedha na sasa kuna nafuu hasa kwenye jimbo la Hirshabelle nchini humo. 

Sauti
4'6"
Laura Quinones

Wanaharakati huko COP27 wasema hakuna hatua kwa tabianchi bila kujali haki za binadamu

Huko Sharm-el-Sheikh nchini Misri, kwenye mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP27, tarehe 17 mwezi huu wa Novemba yalishuhudiwa maandamano ya maelfu ya wawakilishi wa watu wa jamii ya asili, wanawake, wanarahakati wa masuala ya jinsia, vijana, mazingira na haki kwa tabianchi kutoka pande mbalimbali za dunia. Wao waliandamana kwa niaba ya maelfu ya mashirika na mamilioni ya watu  na kupitisho azimio lao la umma kuhusu haki kwa tabianchi. Wanapaza sauti je ni sauti zipi?

Sauti
3'51"
OHCHR Video

Haki za watu wenye ualbino Uganda, sasa zatambulika kisheria, waliowabagua watozwa fedha

Watu wenye ualbino wamekuwa wakikumbwa na changamoto lukuki ikiwemo za kijamii, kiafya na kiuchumi hali inayofanya mustakabali wao kuwa na mashaka na hata wakati mwingine wanakuwa na wasiwasi kuhusu ndoto zao . Lakini kwa mtoto Elizabeth Ayebare ambaye ndoto yake ilikuwa almanusura itumbukie shimoni, mambo sasa ni shwari kwani sheria ilifuata mkondo wake na waliokuwa wanataka kupeperusha ndoto yake wakachukuliwa hatua ya kumlipa fidia na sasa anaendelea na masomo yake kama kawaida. Nini kilifanyika?

Sauti
4'35"
OCHA/ Trond Jensen

Mafuriko Nigeria yaathiri zaidi ya watu milioni 3 na kukatili maisha ya watu 600: OCHA

Mafuriko makubwa yanayoikumba Ningeria hivi sasa hayajawahi kushuhudiwa kwa zaidi ya muongo mmoja limesema Ofisi ya Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA na kuongeza kuwa hadi kufikia sasa zaidi ya watu milioni 3 wameathirika wengine wakipoteza maisha, zaidi ya milioni kutawanywa na miundombinu muhimu ikiwemo nyumba, barabara na mashamba vimesambaratishwa.

Sauti
3'53"