Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN Video

Sikufahamu kuhusu zao la mwani, sasa limenibadilishia maisha yangu- Marinda

Wakati mkutano wa dunia kuhusu bahari umeanza leo huko Lisbon nchini ureno kujadili namna ya kuhakikisha bahari inalindwa ili jamii zinufaike na uchumi utokanao na shughuli za kwenye bahari au uchumi wa buluu sambamba na faida nyingine nyingi, tunaelekea kijiji cha Kibuyuni, eneo la Shimoni, kaunti ya Kwale nchini Kenya kusikia jinsi maisha ya wakulima wa zao la mwani linalolimwa baharini yalivyobadilika baada ya mradi wa shamba la mfano la mwani ulioanzishwa na Taasisi ya Utafiti wa Majini na Uvuvi ya Kenya KMFRI kuleta manufaa kwa wanakijiji zaidi ya 2500 wa kijiji hicho.

Sauti
3'37"
UNHCR Video

Nashukuru Mungu, nashukuru Iran- Mkimbizi kutoka Afghanistan

Iran, taifa hili la Mashariki ya Kati kwa miongo minne sasa limehifadhi zaidi ya wakimbizi 800,000 kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Afghanistan. Wakimbizi wanaowasili kando mwa shida za kusaka hifadhi ili waweze kuendeleza maisha  yao, kuna tatizo la afya.  Gharama za matibabu ni za juu na iwapo mkimbizi ana ulemavu hali inakuwa mbayá zaidi. Hali hiyo imemkumba Sultan Zoori mkimbizi kutoka Afghanistan aliyewasili Iran akiwa kwenye kitimwendo huku akihitaji huduma za afya zenye gharama ya juu. Awali hali ilikuwa si shwari lakini wahenga walinena, Mungu si Athumani, kulikoni?

Sauti
3'34"
© UNICEF/Patrick Brown

Watoto watumikishwao DRC wapaza sauti zao

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 wanatumikishwa kwenye kazi mbalimbali ikiwemo uchimbaji madini, ujenzi wa nyuma, na hata sokoni kwa lengo la kukidhi mahitaji ya familia za kutokana na hali ya umaskini. Mashirika ya kutetea hali ya watoto yanachukua hatua kusihi serikali kuhakikisha sheria za kumlinda mtoto zinazingatiwa ikiwemo kwenye machimbo ya madini. Lakini hali iko vipi , mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa huko DRC, Byobe Malenga amevinjari kwenye mji wa Bukavu jimboni Kivu Kusini ili kujionea hali halisi.
Sauti
3'20"
WHO/L. Pezzoli

Bunge lina nafasi kubwa ya kubadili mwelekeo wa afya ya jamii: Mbunge Nyongo

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limekuwa likizihimiza nchi zote duniani kuhakikisha zinafikia lengo la huduma za afya kwa wote ifikapo mwaka 2030 wakati huu ikiwa imesalia chini ya miaka 10 kufikia ukomo wa malengo hayo. Hata hivyo bado jamii nyingi hasa barani Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara lengo hilo ni mtihani na huenda nchi nyingi zisilifikie kwa asilimia 100 limesema shirika hilo. Je nini ni kikwazo kikubwa cha kufikia lengo hilo? Na serikali pamoja na mihimili yake likiwemo Bunge wanafaya nini kuhakikisha hatua zinapigwa?

Sauti
4'57"
UN News

Kongamano lafanyika Dodoma kujadili sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo Tanzania

Mabadiliko ya tabianchi ni moja ya majanga yanayokumba dunia hivi sasa na kuathiri sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji na uvuvi. Nchini Tanzania kwa kutambua athari hizo hasi, kumefanyika kongamano la nane la mwaka 2022 la  sera kwa wadau wa sekta hizo, kongamano lilofanyika katika mji mkuu wa taifa hilo, Dodoma. 

Washiriki takribani 600 wametoka mikoa na pande mbalimbali ikiwemo shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO Tanzania, serikali na sekta binafsi. 

Sauti
4'18"
UN Women/Ruth McDowall

Tanzania yazindua programu ya malezi, ustawi na makuzi ya watoto katika mikoa 10

Lishe duni ni moja ya changamoto mtambuka hususani katika ustawi na makuzi ya watoto. Kwa kulizingatia hilo na kwa kutambua kuwa kila nchi inapaswa kushiriki katika kuyasongesha malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endekevu, SDGs, Tanzania imezindua programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwa lengo la kumaliza changamoto ya lishe duni na changamoto nyingine dhidi ya watoto hususani walio chini ya umri wa miaka nane.

Sauti
3'37"
© UNDP/Amunga Eshuchi

Kila mtu ana jukumu la kulinda mazingira ya bahari

Ikiwa leo ni siku ya bahari duniani Umoja wa Mataifa unamchagiza kila mtu kuchukua hatua na kulinda mazingira ya bahari ambayo sio tu ni muajiri mkubwa wa sekta ya uvuvi duniani bali ni mdau mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi na kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa duniani kote thamani ya soko la sekta ya bahari na rasilimali zake inakadiriwa kuwa ni dola trilioni 3 kwa mwaka au asilimia 5 ya pato la dunia ndio maana unaichagiza dunia kushikama kuchukua hatua kuilinda bahari kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho.

Sauti
4'10"
FAO Tanzania

FAO na SIDO Tanzania yapatia mama lishe mafunzo ya usalama wa chakula

Tarehe 7 mwezi Juni kila mwaka ni siku ya usalama wa chakula duniani, ambapo Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la chakula na kilimo FAO, unaangalia ni kwa jinsi gani chakula kinaweza kuwa ni bora kwa mlaji bila kuathiri afya yake kuanzia shambani hadi mezani. Nchini Tanzania, FAO  imeshirikiana na shirika la viwanda vidogo nchini humo, SIDO na kupatia mafunzo mama na baba lishe katika majiji mawili ya mkoa wa Dodoma na DAr es salaam. Kulikoni?

Sauti
4'5"