Manusura wa usafirishaji haramu binadamu Ethiopia wasimulia yaliyowasibu
Tarehe 30 mwezi Julai kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu duniani. Umoja wa Mataifa unasema mwaka 2018 watu 50,000 walibainika katika 148 kuwa wamesafirishwa kiharamu. Asilimia 50 ya watu hao wanatumikishwa kingono ilhali asilimia 38 ni utumikishaji kwenye ajira.