Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNCDF wamenipatia elimu na kuniunganisha na taasisi za kifedha – Mkurugenzi Nabuhima Foods  

UNCDF wamenipatia elimu na kuniunganisha na taasisi za kifedha – Mkurugenzi Nabuhima Foods  

Pakua

Aaron Mwimo kwa jina la utani Joti, ni mmoja wa watu wanaochangia utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs kwa kuleta ustawi bora kwa jamii yake wilayani Kibondo, mkoa wa Kigoma nchini Tanzania.  

Bwana Mwimo alianzisha kiwanda kidogo cha kuchakata mazao ya wakulima kama vile mahindi na mihogo na akakipa kiwanda chake kidogo jina Nabuhima Food Supplies akisambaza unga katika mji eneo dogo la mji wa Kibondo hadi pale alipounganishwa na shirika la mitaji la Umoja wa Mataifa.  

Shirika la mitaji la Umoja wa Mataifa UNCDF lilisaidia kiwanda hicho kujenga ghala mbili za kuhifadhia maji na kuweka mfumo wa maji ya bomba kiwandani, hali ambayo imesaidia kupunguza umaskini na kuongeza ajira si tu kwa wakazi wa maeneo jirani na kiwanda hicho bali pia mbali zaidi. Anold Kayanda ameufuatilia mradi huo na kuandaa makala ifuatayo. 

Audio Credit
UN News/Anold Kayanda
Audio Duration
4'58"
Photo Credit
UNCDF