Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanafunzi wapatiwa elimu ya namna ya kuishi na watu wenye ualbino

Wanafunzi wapatiwa elimu ya namna ya kuishi na watu wenye ualbino

Pakua

Mtoto umleavyo ndio akuavyo ni methali unaofundisha jamii kuhakikisha iwapo inataka watoto wawe na tabia fulani basi ni vyema waanze kuwafundisha wangali wadogo. Na ndicho kinachofanywa nchini Tanzania na Chama cha watu wenye ualbino TAS mkoa wa Morogoro, mashariki mwa taifa hilo. 

Chama hicho kinaendelesha programu ya kutoa elimu kwa wanafunzi na kimetembelea shule ya msingi kilakala iliyopo Manispaa ya Morogoro na kutoa elimu kwa wanafunzi wa darasa la sita na la saba juu ualbino na namna ya kuishi nao katika Jamii.

Miongoni mwa kilichowasukumua kutoa elimu kwa wanafunzi hao ni kuwa wanatumaini pindi wanfunzi watakapopata elimu hiyo wataenda kuwaelimisha na wengine na hii inaweza kuleta uelewa zaidi kwa Jamii hasa kwa watoto wenyewe kwa wenyewe wakikutana.

Tuungane na Sure Ndereka wa Redio washirika Mviwata fm aliyeshuhudia wanafunzi hao wakipatiwa mafunzo na kutuandalia makala hii

Audio Credit
Leah Mushi/Sure Ndereka
Audio Duration
3'23"
Photo Credit
UNICEF