Wakati napigana msituni sikuweza kutunza familia, sasa mradi wa MONUSCO umeniinua- Aristote
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hali ngumu ya maisha inatumbukiza vijana katika mapigano ya msituni mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu. Kwa kubaini hilo, Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo MONUSCO unatekeleza miradi kama ule wa kuvunja makundi yaliyojihami, kupokonya silaha wanamgambo na kuwajumuisha kwenye jamii, DDR, mradi ambao unatamatishwa kwa kuwapatia wapiganaji hao wa zamani stadi za maisha ili wajipatie kipato.