Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UNMISS

UNMISS yawajengea uwezo wafanyabiashara nchini Sudan Kusini

Ushirikiano na ukuaji kiuchumi ni miongoni mwa masuala muhimu katika kuhakikisha nchi yoyote ina amani na wananchi wake wanapata Maendeleo. Na ili kuhakikisha wananchi wa Sudan Kusini wana amani na maendeleo, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani nchini humo UNMISS umeandaa warsha ya biashara lengo likiwa ni kuwatia moyo wafanyabiashara wa ndani na kuwawezesha kiuchumi ili nao waweze kuimarisha biashara zao lakini pia waweze kufanya biashara na Umoja wa Mataifa .

Sauti
3'34"
UNCDF Tanzania

UNCDF yawanufaisha wakulima wa viazi lishe Mkoani SIMUYU

Tarehe 24 Oktoba dunia ilisherehekea siku ya Umoja wa Mataifa kwa kuadhimishwa miaka 77 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1945. Ingawa kuanzishwa kwake kuliangalia zaidi masuala ya Amani na usalama na Haki za Binadamu lakini Shirika hili kubwa la kimataifa limezidi kupanua wigo wake na sasa wanashiriki katika sekta zote duniani, lengo likiwa ni kuboresha maisha ya watu wote na kuhakikisha wana ustawi wa maisha na pale kwenye changamoto shirika husika la Umoja wa Mataifa hutafuta ufumbuzi.

Sauti
6'5"
Benki ya Dunia/ Screenshot

Mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania yachukua hatua kukabili madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa watoto

Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kubainishwa kila uchao. Mathalani hivi karibuni ripoti ya mashirika ya Umoja wa Matiafa ilitaja kuwa watoto milioni 559 kwa sasa wanakabiliwa na joto Kali na hali inategemewa kuwa mbaya zaidi ambapo mpaka kufikia mwaka 2050 watoto wote duniani ambao wanakadiriwa kuwa bilioni 2.02 watakumbwa na madhara ya joto kali. Joto kali ni moja ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
4'11"
UNICEF Zambia

Mradi wa UN Zambia warejesha watoto wa kike shuleni, wazazi wafurahia

Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake lile la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA na la kuhudumia watoto, UNICEF  huko nchini Zambia unatekeleza mradi wa kuchochea kasi ya kutokomeza ndoa za utotoni, GPECM. Mradi unalenga kulinda na kuendeleza watoto wa kike na barubaru ili kuzuia mimba na ndoa za utotoni na hatimaye wafikie malengo ya juu ya ustawi kielimu, kiuchumi na kijamii.

Sauti
4'23"
Benki ya Dunia

Jamii ilinishangaa nilipoamua kusomea kuchomelea vyuma sababu mimi ni msichana

Tatizo la ajira hususan kwa vijana ni suala linaloumiza vichwa kuanzia ngazi ya familia, kitaifa mpaka kimataifa. Nchini kenya katika kusaka suluhu ya tatizo hili Serikali ya Kenya imeanzisha mradi wa Ajira na Fursa kwa vijana au KYEOP unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ukilenga vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 mpaka 29 ambao wanapatiwa fursa ya elimu ili waweze kuajirika au wakishahitimu na kufungua biashara zao waweze kutengeneza fursa za ajira kwao na kwa wengine.

Sauti
4'
UN News Kiswahili

Kunywa maziwa kuimarisha afya yako: FAO Tanzania

Tarehe 16 mwezi Oktoba kila mwaka dunia inaadhimisha siku ya chakula dunia, mwaka huu wa 2022 kauli mbiu ni Uzalishaji bora, lishe bora, mazingira bora, na maisha bora kwa wote :Habaki mtu nyuma” Kauli mbiu hii inaakisi hali halisi ya ulimwengu tunaoishi kwani kwa sasa kila pembe ya Dunia kuna changamoto mbalimbali kuanzia za mabadiliko ya tabia nchi mpaka vita vyote hivi vikipandisha bei za bidhaa na vyakula mara dufu na hii inasababisha jamii nyingi kujikuta hazina uhakika wa chakula.

Sauti
4'6"
UN NEWS/ Anold Kayanda

Nchi ya Somalia yaomba kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki

Nchi ya Somalia imeomba kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dkt. Peter Mathuki alipokuwa hapa jijini New York Marekani ambapo alifanya mazungumzo na Leah Mushi wa idhaa hii.

Dkt. Mathuki anaanza kwakueleza jumuiya hiyo sasa ina wanachama wangapi. 

Sauti
2'25"
UN News

Kuhakikisha afya ya mtoto, Tanzania yatekeleza programu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto

Mashiriki 77 yasiyo ya kiserikali mkoani Morogoro, Tanzania yameanza kunufaika na mradi jumuishi wa kitaifa unaofahamika kwa kifupi MMMAM yaani Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto. Programu ya MMMAM inasimamiwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau kama  Shirika lisilo la kiserikali la Community Development Organization (CDO).

Kutoka Morogoro, Tanzania, Mwandishi Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM ya Morogoro Tanzania ametuandalia makala hii kuhusu mradi huo. 

 

Sauti
3'36"