Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwalimu Neema atengeneza vifaa vya kuwezesha watoto kuelewa anachofundisha.

Mwalimu Neema atengeneza vifaa vya kuwezesha watoto kuelewa anachofundisha.

Pakua

Hii leo ni siku ya walimu duniani na ujumbe ni ujumbe marekebisho  ya mfumo wa elimu huanza na mwalimu. Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO linasema lengo la ujumbe huo  ni kusherehekea dhima muhimu ya walimu katika uwezo wa wanafunzi kwa kuhakikisha wana vifaa na mbinu zinazowawezesha za kujiwajibikia wao wenyewe na watu wengine. UNESCO inataka serikali ichukue hatua kuhakikisha walimu wana mbinu, lakini huko Tanzania, Mwalimu mmoja ameona asisubiri bali achukue hatua kwa kutengeneza hata vile vifaa vya kufundisha ili wanafunzi waweze kuelewa. Je nini kinafanyika? Hamad Rashid wa Radio washirika MVIWATA FM ya mkoani Morogoro mashariki mwa TAnzania amefunga safari hadi kwa Mwalimu Neema. Kwako Hamad.

Audio Credit
Assumpta Massoi/ Anold Kayanda
Audio Duration
3'49"
Photo Credit
UN News