Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Makala Maalum

Baraza Kuu lilipitisha azimio mwaka 2012 lililoipa Palestina hadhi ya kuwa nchi isiyokuwa mwanachama katika Umoja wa Mataifa. (faili)
UN Photo/Rick Bajornas

Hadhi ya Palestina ndani ya UN yafafanuliwa 

Je, itachukua nini kwa Palestina kuwa Nchi Mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa? Wakati Baraza la Usalama linashughulikia suala hilo wakati vita vya uharibifu huko Gaza vikiingia mwezi wake wa saba, tuliangalia hali ya sasa ya Palestina na kile kinachohitajika kuwa Nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Mwanamke akiwa na mtoto wake mchanga akiwasikiliza wafanyakazi wa UNFPA katika kikao cha kuongeza uelewa kuhusu ukatili wa kijinsia katika Kituo cha One Stop katika Hospitali ya Sominé Dolo.
© UNFPA Mali/Amadou Maiga

Safari hatari na isiyo salama ya wajawazito nchini Mali

Aissata Touré, mwenye umri wa miaka 16, ndio kwanza amejifungua mtoto wake wa kwanza. Mama huyu ambaye naye ni mtoto, alikuwa na matumaini ya kjifungulia karibu na kijiji chao cha Ngouma nchini Mali, lakini mhudumu wa afya alimshauri aende hospitali kutokana na uwezekano wa kupata tatizo wakati wa kujifungua. Ilikuwa safari yenye changamoto na gharama kubwa.