Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mlinzi wa majengo ya UM Usomali auawa

UM imeripoti Ijumanne majambazi kadha walimpiga risasi na kumwua ofisa raia wa usalama nchini Usomali, aliyekuwa akitumikia Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP), kitendo kilichotukia kwenye mji wa Beledweyn, Usomali.

Hali Chad Mashariki yazidi kuharibika, kuhadharisha OCHA

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imeripoti hali ya usalama katika Chad Mashariki inaendelea kuwa mbaya zaidi. Mnamo mwisho wa wiki iliopita, msafara wa UM wa magari matatu ya kiraia, wa Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika Jamuri ya Afrika ya Kati na Chad (MINURCAT) uliohusika na ugawaji wa misaada ya kihali kwa umma waathirika wa mapigano, ulishambuliwa na majambazi wasiojulikana wanane. Ofisa mmoja wa Vikosi vya Ulinzi wa Mchanganyiko, aliyekuwa akiongoza msafara wa UM, alijeruhiwa.

Hapa na pale

Msafara wa Shirika la UM juu ya Amani katika Jamhuri ya AfrIka ya Kati na Chad (MINURCAT), unaohusika na ugawaji wa vitu na watu, uliojumuisha magari ya kiraia matatu, ulishambuliwa Ijumapili na watu wanne wasiotambulika waliochukua silaha, kwenye eneo la kusini-mashariki katika Chad. Vikosi vya MINURCAT vilipelekwa haraka kwenye eneo, pamoja na wahudumia tiba ili kuokoa watumishi waliopatwa na ajali hiyo, pamoja na kuyaokoa magari ya MINURACT yalioharibiwa na mashambulio.

Ripoti ya fujo Guinea yakabidhiwa makundi husika na KM

Msemaji wa KM ameripoti kwamba Ban Ki-moon leo amewatumia makundi kadha husika na tukio la Guinea, ripoti maalumu ya Tume ya Uchunguzi ya Kimataifa juu ya hatua kali za kinidhamu zilizochukuliwa na vikosi vya usalama dhidi ya raia waliokuwa wakiandamana, bila ya fujo, kwenye mji wa Conakry, mnamo mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu, ambapo raia wanaokadiriwa 150 waliuawa, na wingi kujeruhiwa.

Hapa na Pale

Tarehe ya 18 Disemba huadhimishwa na UM kuwa ni Siku ya Kimataifa kwa Wahamaji. Risala ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), iliowasilishwa kuadhimisha siku hii, ilihimiza mataifa kuonyesha bidii za mbele zaidi, kupita Mkutano wa Copenhagen, na kukabili masuala magumu ya uhamaji unaochochewa na uharibifu wa mazingira na uchafuzi wa hali ya hewa. Taarifa ya IOM ilieleza wanasayansi wa kimataifa walishathibitisha kihakika kwamba mabadiliko ya hali ya hewa na uchafuzi wa mazingira ni mambo yanayozusha uhamaji wa dharura na kusababisha watu kung\'olewa mastakimu, katika sehemu mbalimbali za dunia, hasa katika nchi masikini, maeneo ambayo ndio yenye kudhurika zaidi na maafa ya kimaumbile. Kwa mujibu wa IOM kuna pengo kubwa la maarifa na uzoefu juu ya ujuzi unaofaa kushughulikiwa, ili kudhibiti vyema matokeo na athari kubwa za uhamaji unaoletwa na maafa ya kimazingira.