Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Waasi wa LRA walihusika na mauaji ya raia katika JKK, OCHA imethibitisha

Vile vile kuhusu JKK, Elizabeth Byrs, Msemaji wa Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) ametoa taarifa yenye kuthibitisha ya kuwa baina ya tarehe 1 hadi 20, Januari mwaka huu, waasi wa Uganda wa kundi la LRA waliosakama katika JKK, walishambulia mitaa 19 katika wilaya ya Haut Uele, kwenye jimbo la Orientale na kuua raia 269, na baadaye kufanya uharibifu wa mali, na kuiba pamoja na kuchoma moto nyumba za raia.

Hapa na Pale

KM ameripotiwa kukaribisha, kwa matumaini ya kutia moyo, uamuzi wa chama cha upinzani cha MDC kujiunga na serikali ya umoja wa taifa ya Zimbabwe, kama ilivyoidhinishwa kwenye Mapatano ya Amani ya 15 Septemba 2008 pamoja na mapendekezo ya Viongozi wa SADC ya 27 Januari 2009. UM imesema itafanya kila iwezalo na kuahidi mchango kamili utakaosaidia Mapatano ya 15 Septemba kutekelezwa nchini Zimbabwe kama inavyotakiwa. KM ameisihi Serikali ya Zimbabwe kuchukua kila hatua zinazohitajika kukabiliana na mizozo ya kiutu na kiuchumi ilioselelea nchini, na vile vile kuitaka ihishimu mifumo ya uhuru wa kidemokrasia katika nchi.

KM atoa mwito wa kufadhiliwa dola milioni 613 kuhudumia Ghaza

Hii leo kutoka mji wa Davos, Uswiss – palipojumuika viongozi wa dunia kuzingatia masuala ya kufufua uchumi wa kimataifa – KM Ban Ki-moon alianzisha kampeni ya kuwaomba wahisani wa kimataifa kuchangisha, kidharura, dola milioni 613, zinazohitajika kuisaidia UM kuhudumia kihali na mali umma wa Tarafa ya Ghaza, ulioathirika na gharika na uharibifu wa wiki tatu wa eneo lao kutokana na mashambulio ya vikosi vya Israel.

Wanakijiji 100 wauawa na LRA katika JKK

Liuteni Kanali Jean-Paul Dietrich, Msemaji wa Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) amenakiliwa akisema kwamba maiti karibu 100 ziligunduliwa karibuni katika jimbo la Orientale, kaskazini-mashariki ya JKK.

Mpatanishi wa UM/UA kwa Darfur asisitiza mapigano mapya yakomeshwe halan

Kwenye taarifa rasmi iliotolewa mjini Khartoum, Sudan na Djibril Bassolé, Mpatanishi wa Pamoja wa UM/UA kuhusu mpango wa amani kwa Darfur, ilidhihirisha wasiwasi wake juu ya kurudiwa tena kwa mapigano katika eneo la kusini, hali ambayo, alionya, kama haijadhibitiwa mapema itadhoofisha zile juhudi za kurudisha utulivu na amani kieneo, kwa kulingana na Mapatano ya Kiutu ya 2004 ya Kusimamisha Mapigano katika Darfur.