Hapa na pale
John Holmes, KM juu ya Masuala ya Kiutu na Misaada ya Dharura ameshtumu, kwa kauli kali, mashambulio ya raia yaliofanyika karibuni kwenye jimbo la Kivu Kusini, katika JKK, na kundi la waasi la FDLR.
John Holmes, KM juu ya Masuala ya Kiutu na Misaada ya Dharura ameshtumu, kwa kauli kali, mashambulio ya raia yaliofanyika karibuni kwenye jimbo la Kivu Kusini, katika JKK, na kundi la waasi la FDLR.
Alkhamisi Baraza la Usalama asubuhi lilianza shughuli zake kwa kujadilia hali katika Cyprus, na maendeleo kuhusu mazungumzo ya kusawazisha mfarakano baina ya raia wa Kigiriki na wale wa Kituruki.
Alan Doss, Mjumbe Maalumu wa KM kwa JKK ameyakaribisha maamuzi ya mahakama ya kijeshi la taifa ya kuwatia hatiani maofisa 20 wa jeshi, waliotuhumiwa kushiriki kwenye makosa yanayojumlisha wizi wa mabavu, jinai dhidi ya utu na vitendo haramu vya kunajisi raia kihorera.
Wataalamu wa sayansi 600 kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika wiki hii Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria Kikao cha Awali cha Kamati ya Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia (CODIST-1) kilichoanza mashauriano leo Alkhamisi.
Dktr Keiji Fukuda, Mkurugenzi Mkuu Mwandamizi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kwenye mahojiano Alkhamisi na waandishi habari mjini Geneva, alitangaza takwimu mpya juu ya maambukizo ya homa ya mafua ya nguruwe, ambayo kuanzia leo itajulikana rasmi kama homa ya vimelea vya H1N1.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti idadi ya watu walioambukizwa na maradhi ya homa ya mafua ya nguruwe imeongezeka, kwa kulingana na taarifa ilizopokea Ijumatano kutoka maabara ya uchunguzi wa kisayansi wa maradhi.
Shirika la UM Kuhudumia Matrumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) limetangaza kuwa limepokea orodha rasmi ya wagombea uchaguzi wa cheo cha Mkurugenzi Mkuu mpya wa taasisi hii ya kimataifa baada ya kiongozi wa sasa Mohamed ElBaradei kutangaza atastaafu atakapomaliza muda wake mwaka huu.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Marekani ya Kudhibiti Maradhi (CDC) amenakiliwa na vyombo vya habari akithibitisha ripoti inayosema mtoto mchanga wa miezi 23, katika jimbo la Texas, amesajiliwa kufariki kufuatia maambukizo ya homa ya mafua ya nguruwe. Kifo hiki ni cha kwanza kutukia Marekani, miongoni mwa wale watu waliopatwa na ugonjwa huo.
Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limekanusha kihakika tetesi za ripoti ya shirika la habari la Uingereza la BBC zinazodai John Bosco Ntaganda, mtuhumiwa wa jinai ya vita na kiongozi wa kundi la waasi la CNDP kwenye eneo la kaskazini-mashariki ya JKK, alishiriki kwenye operesheni za vikosi vya UM nchini mwao.
KM wa UM Ban Ki-moon ameyasihi Mataifa Wanachama kuchukua hadhari kuu ili kuhakikisha silaha maututi za kemikali hazitodhibitiwa katu na makundi ya magaidi. KM aliyasema haya kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kuwakumbuka Waathirika wa Mapigano Yanayotumia Kemikali.