Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hapa na Pale

Tume ya Kuchunguza Ukweli juu ya Vita katika Tarafa ya Ghaza, iliobuniwa rasmi mwezi uliopita kwenye kikao maalumu cha Baraza la Haki za Binadamu Geneva, inatarajiwa kuelekea Ghaza mnamo mwisho wa wiki hii, kwa kupitia kivuko cha Rafah, kiliopo upande wa Misri. Tume ya watu watatu, inayoongozwa na Jaji Richard Goldstone wa Afrika Kusini, itawasili Ghaza Juni mosi na itakutana na makundi husika yote na mgogoro wa eneo hilo, ikijumlisha mashirika yasio ya kiserikali, jumuiya za kiraia, mashirika ya UM, waathirika wa mashambulio ya Israel pamoja na kuklutana na wale mashahidi wengine wanaohusika na madai ya kufanyika ukiukaji wa haki za kibinadamu katika eneo liliokaliwa. Tume ya Barazala Haki za Binadamu pia itakutana na watu wengine wenye taarifa ziada juu ya ukweli wa matukio yanayofanyiwa uchunguzi katika Ghaza.

Hapa na pale

Asubuhi, Baraza la Usalama lilifanyisha mkutano kusailia hali katika Bosnia na Herzegovina. Wajumbe wa Baraza walipatiwa fafanuzi juu ya maendeleo ya kurudisha “utulivu na usimamizi wa utawala wa muda mrefu” kieneo, kutoka Mjumbe Mkuu mpya wa UM kwa Bosnia na Herzegovina, Valentin Izko. Alisema hali katika miezi sita iliopita nchini Bosnia-Herzegovina ilikuwa “imara na isio wasiwasi” lakini umoja wa taifa, katiba na mfumo wa kiTaifa ni masuala ambayo bado yanaendelea kupigwa vita na Republika Srpska, eneo la nchi ambalo limeashiria linataka haki ya kujiamulia wenyewe na kujitenga. Na mnamo alasiri Baraza la Usalama lilifanyisha kikao rasmi juu ya ziara ya karibuni ya wajumbe wa Baraza katika JKK, Rwanda, Liberia na Ethiopia, ambapo walipata fursa ya kushauriana na wawakilishi wa Umoja wa Afrika (UA).

WFP yafungua ofisi mpya Usomali ya Kati

Shirika la Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limefungua ofisi mpya katika eneo la Usomali ya Kati. Hatua hii muhimu iliochukuliwa na UM inatarajiwa kurahisisha shughuli za kuhudumia chakula watu muhitaji milioni moja ziada, waliokuwa wakitegemea shirika lisio la kiserikali, ambalo liliondoka nchini mwaka jana, kwa sababu ya ukosefu wa usalama wa wafanyakazi.