Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hapa na Pale

Kwenye mkutano wa hadhara, asubuhi, na watumishi wa UM, KM Ban Ki-moon alisema mgogoro uliopamba sasa hivi katika Tarafa ya Ghaza, na pia Israel kusini, umesasbabisha uharibifu zaidi katika saa 48 zilizopita. Alisema mateso na maumivu yaliowakumba raia yanashtusha, na alisisitiza operesheni za vikosi vya Israel zilizoanzishwa Ijumamosi ndani ya Ghaza yenyewe, zimeharibu kabisa hali katika eneo hilo.~

BU na KM wasailia hali baada ya kuingia Ghaza kwa majeshi ya Israel

KM Ban Ki-moon, kwenye taarifa iliotolewa na msemaji wake, alinakiliwa akisema ameingiwa na “wasiwasi mkubbwa kuhusu athari mbaya kufuatia kuanzishwa kwa operesheni za ardhini za vikosi vya Israel katika Tarafa ya Ghaza” Ijumamosi (03/01/2009), wakati ambao Baraza la Usalama (BU) vile vile liliamua kuitisha kikao cha dharura kuzingatia hali hiyo ya uhasama Ghaza.

UNRWA yaomba dola milioni 34 kuhudumia misaada ya kiutu katika Ghaza

Shirika la UM Linalofarajia Wahamiaji wa KiFalastina katika Mashariki ya Karibu (UNRWA) limetoa ombi kwa wahisani wa kimataifa la kufadhiliwa msaada wa dharura wa dola milioni 34, ili kukidhi, halan, mahitaji ya umma wa Tarafa ya Ghaza, mahitaji ambayo yanaendelea kukithiri tangu mashambulizi kuanzishwa na vikosi vya Israel kwenye eneo mnamo tarehe 27 Disemba 2008.~~

MONUC yakataa hadharani madai ya Nkunda

Shirika la UM juu ya Ulinzi Amani katika JKK (MONUC) limeripoti kukanya madai ya Laurent Nkunda, kiongozi wa kundi la waasi wa CNDP aliyoyabainisha kwenye barua aliomtumia Mjumbe Maalumu wa KM, Alan Doss, madai yaliyosema kwamba vikosi vya Serikali vimeonekana kuongezwa kwenye ile sehemu ya mapigano, katika eneo la mashariki la Kibati, liliopo kilomita 10 kaskazini ya mji wa Goma.

SALAMU ZA MWAKA MPYA

WASIKILIZAJI, ALKHAMISI YA LEO, TAREHE MOSI JANUARI 2009, OFISI ZOTE ZA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA MATAIFA MJINI NEW YORK ZIMEFUNGWA, KUADHIMISHA SIKU KUU YA MWAKA MPYA.~