Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Siku ya UN, wakimbizi Uganda wapaza sauti

Ikiwa leo ni siku ya Umoja wa Mataifa, makundi mbalimbali yamezungumzia kile ambacho chombo hicho kinawasaidia katika zama za sasa zilizogubikwa na changamoto lukuki. Umoja wa Mataifa wenye wanachama 193 unahakikisha kuwa rasilimali kidogo iliyopo inatumika kuleta maisha bora hata kwa watoto na vijana wakimbizi ambao kwao maisha ni machungu na hivyo wamekimbilia ugenini. Mfano ni nchini Uganda ambako katika siku hii ya Umoja wa Mataifa, John Kibego amevinjari na kuzungumza nao.

Sauti
3'23"
©FAO/Amos Gumulira

Mkulima kutoka Kagera asimulia FAO Tanzania ilivyomkomboa

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limeendelea na harakati zake za kusaidia nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinafanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan namba 1 la kutokomeza umaskini na lile la pili la kutokomeza njaa. Mfano huko  nchini Tanzania hususan mkoani Kagera FAO imefungua fursa kwa jamii kama vile wanawake kujikwamua kimapato kupitia kilimo. Fursa hiyo imedhihirika kwa mmoja wa wakulima ambaye ametembelewa na Nicolaus Ngaiza wa radio washirika Kasibante FM mkoani Kagera nchini Tanzania.

Sauti
3'51"
UN

Ethiopia yaazimia kuondokana na DDT, UNEP yaipatia msaada

DDT kemikali yenye sumu iliyolenga kuangamiza wadudu waharibifu wa mimea na hata wanaosambaza ugonjwa wa Malaria yaani mbu imebainikuwa pale inapotumika husalia ardhini na kuharibu siyo tu mazingira bali pia afya ya binadamu na Wanyama.

Tayari nchi nyingi zimepiga marufuku matumizi ya DDT ilhali zingine zikiona bado zina uwezo wa kuitumia bila madhara yoyote. Kwa zile ambazo zimeamua kuteketeza maelfu ya tani ya DDT, shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, limeamua kuzisaidia na miongoni mwao ni Ethiopia.

Sauti
3'41"
(Picha: Idhaa ya Kiswahili/Grace Kaneiya)

Sote tuwe wainjilisti wa dunia yenye mazingira bora- Rocky

Nyota ya mwanamuziki mashuhuru kutoka Ghana, Rocky Dawuni inazidi kung'ara  katika anga za kuchechemu dunia kutekeleza yale yaliyo bora kwa maslahi ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. Mwanamuzi huyu ambaye amekuwa akitumia kipaji chake cha kuimba kupazia sauti masuala yanayoweka hatarini mustakabali wa binadamu, amezidi kuonekana na hata kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa taasisi mbali mbali ikiwemo zile za Umoja wa Mataifa.

Sauti
2'47"

Wakulima tumenifaika na mradi wa FAO

Kwa msaada wa Muungano wa Ulaya, EU, Shirika la chakula na kilimo duniani FAO mwaka 2015 lilianzisha mafunzo ya kilimo bora kinachohifadhi mazingira kwa wakazi wa kaunti nane nchini Kenya. Lengo ni kuwasaidia wakulima hao kuongeza uzalishaji wa mazao na pia kuwaunganisha na masoko ya uhakika na  hatimaye kuweza kupunguza umaskini, kutokomeza njaa na hata kuboresha lishe ya familia.  Je nini kilifanyika? Grace Kaneiya anasimulia zaidi katika makala haya yaliyowezeshwa na FAO.

Sauti
2'15"

Umaskini bado ni changamoto kwa baadhi ya wananchi wa Burundi

Leo ikiwa ni siku ya kutokomeza umaskini duniani, ambalo ni lengo la kwanza la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs Umoja wa Mataifa unasema bado watu milioni 700 kote ulimwenguni wanaishi kwenye lindi la umaskini, bila kufahamu mlo wao wa kesho utatoka wapi, bila kuwa na uhakika pia wa kipato cha kuwezesha familia kukimu mahitaji mengine muhimu ya kila siku.

Sauti
4'1"

Kilimo bora chaimarisha kipato cha kaya Vietnam

Kilimo ni shughuli inayoleta maendeleo siyo tu kwa kijiji, eneo au taifa kwa ujumla bali pia kwa mtu binafsi na familia yake. Ni kwa kuzingatia hilo, Umoja wa Mataifa umekuwa kila mara unakipigia upatu na kukijumuisha katika ufanikishaji wa  baadhi ya  malengo ya maendeleo endelevu, kama vile malengo namba moja la kuondoa umaskini na pia namba 2 la kutokomeza njaa bila kusahau lengo namba nane  la  kazi nzuri na ukuaji wa kiuchumi na vilevile   usawa wa kijinsia ambalo ni lengo namba tano.

Sauti
2'52"
UNHCR/Antwan Chnkdji

Kutoka maisha ya dhiki hadi zulia jekundu Ufaransa

Maisha ya mtoto Zain mwenye umri wa miaka 13 ni hadithi ya kweli ya kusisimua. Yeye pamoja na familia yake waliikimbia nchi yao ya Syria zaidi ya miaka 7 iliyopita na wakaanza maisha ya mateso ukimbizini Lebanon.

Hadithi yake inaelekea kuwa na mwisho mzuri baada ya kuigiza katika filamu inayoitwa Caphernaum na ambayo hivi karibuni imepata Tuzo nchini Ufaransa.

Zain ameondoka katika mateso, ametembea juu ya zulia jekundu kuipokea Tuzo ya Cannes na kwa msaada wa UNICEF, familia yake imepatiwa makazi nchini Norway ambako ataenda kutimiza ndoto yake ya kuwa msomi.

Sauti
2'36"