Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Ukitaka kuhama tafuta viza hama kihalali- wimbo Fela wa Degg J

Uhamiaji ni suala ambalo linaibua hisia tofauti kwa jinsi linavyochukuliwa na watu tofauti. Wakati uhamiaji unatoa fursa na faida kwa wanaohama na wenyeji wanakofikia lakini kuna changamoto nyingi katika uhamiaji.

Safari hatarishi wanazochukua wahamiaji zinawaweka katika mikono ya wasafirishaji haramu na hatari ya kupoteza hata maisha. Wimbo wa Degg J unatoa taswira ya safari hatarishi hususanzinazochukuliwa na vijana ili kutimiza ndoto zao. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala ifuatayo.

Sauti
4'2"

Ugonjwa wa TB si kulogwa, muhimu ufuate masharti ya matibabu -DJ Choka.

Ripoti ya Shirika la Afya Duniani WHO iliyotolewa hivi karibuni inaonyesha kuwa ugonjwa wa Kifua Kikuu  ndio unaongoza kwa kuwa ugonjwa hatari zaidi wa kuambukiza duniani. Takwimu za hivi karibuni zaidi za Umoja wa Mataifa zinasema kuwa hivi sasa watu milioni 10.4 duniani kote wameambukizwa ugonjwa huo huku milioni 1.6 wakifariki dunia kila mwaka. Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la afya .WHO linataka mbinu mtambuka za kuondokana na ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030.

Sauti
3'27"
UN Photo/Mark Garten)

Naona mustakabali mkubwa ambao unaongozwa na vijana-Restless Development

Umoja wa Mataifa Jumatatu hii umezindua mkakati wake mpya kuhusu vijana ukilenga kuimarisha mchango wa takribani vijana bilioni 2 duniani  kwa lengo la  kukuza amani, uadilifu pamoja na kuwa na  dunia endelevu. Mkakati huo umepatiwa jina,  “Vijana 2030:Mkakati wa  Umoja wa Mataifa  kwa vijana,”  umeshuhudiwa  na viongozi wa nchi na wakuu wa serikali, lakini pia vijana ambapo mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo la kihistoria kutoka shirika la kiraia la Restless Development amezungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii punde tu baada ya tuk

Sauti
3'48"
UN

Viongozi wa sasa waige mfano wa Mandela- Dkt. Salim

Mwendazake Mzee Nelson Mandela, angalikuwa anatimiza umri wa miaka 100 mwaka huu iwapo angalikuwa hai. Ingawa hayupo, bado kile alichokifanya wakati wa uhai wake kinakumbukwa na kuenziwa siyo tu nchini mwake na barani Afrika bali pia katika Umoja wa Mataifa ambako ajenda alizokuwa anatetea ni mambo ambayo ni msingi wa Umoja wa Mataifa.

Sauti
4'31"
FAO/Cristina Aldehuela

Wanawake Burundi wapata mwamko kujiendeleza kiuchumi

Huko Burundi, wanawake wameanza kuchangamkia biashara ndogondogo ili kustaawisha  familia zao.Takwimu zinaonyesha kuwa asimilia 53 ya raia wa nchi hiyo ya Burundi ni wanawake, lakini bado  changamto kubwa ni umaskini unaowazingira sehemu  kubwa ya wanawake hao pamoja  na shida za  kiuchumi. 

Sauti
4'14"
Kwa hisani ya Sheilla Akwara

Nilimeza zaidi ya vidonge 80 ili nijiue-Sheila

Takriban watu laki nane hufariki dunia kila mwaka kutokana na kujiua. Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni ya shirika la afya ulimwenguni WHO, kujiua ni sababu kuu ya pili miongoni mwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 29 kote ulimwenguni.

Kujiua ni janga la dunia huku asilimia 79 ya vifo WHO vilivyotokana na kujiua mwaka 2016 vikitokea katika nchi zenye kipato cha chini na cha wastani.

Sauti
4'18"
UN Photo.

Wanawake nao wazidi kung’ara kwenye urushaji mateke

Mara nyingi imekuwa vigumu sana kwa watu kuweza kuhusisha michezo na Umoja wa Mataifa wakidhani kuwa suala hilo halina nafasi kwenye chombo hicho chenye wanachama 193. Kutokana na fikra hizo mwaka 2001 Umoja wa Mataifa ulianzisha ofisi mahsusi ya michezo kwa ajili ya maendeleo na amani. Lengo ni kipigia chepuo suala la michezo ukisema ya kwamba michezo siyo tu inaleta pamoja watu mahasimu bali pia inaongeza kipato.

Sauti
4'24"
FAO/Olivier Asselin

FAO Tanzania na harakati za kuinua wakulima mkoani Kigoma

Nchini Tanzania, Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake unatekeleza mpango wa pamoja wa kuchagiza maendeleo mkoani Kigoma ukiwa unalenga maeneo kadhaa. Maeneo hayo ni pamoja na kilimo ambamo kwacho wakulima wanapatiwa mbinu za kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabia nchi lakini pia kilimo na ufugaji unaoimarisha lishe kwa kaya.

Sauti
4'7"