Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN News

'Hatuhamihami" bali tunahama na tutarejea- Dkt. Laltaika

Mvutano mkubwa huibuka baina ya wakulima na jamii ya watu wa asili hususan ile ya wafugaji. Mvutano huo ni katika masuala ya matumizi ya ardhi ambapo mara nyingi wafugaji hulaumiwa kutumia ardhi kiholela kutokana na kuhama kwao wanaposaka malisho ya mifugo yao. Umoja wa Mataifa unasisitiza masuala ya matumizi bora ya ardhi kama njia ya kulinda tabianchi Je ni kweli wafugaji  huhamahama? Na je kupitia wafugaji hasa wa jamii ya asili ,dunia inaweza kubadili mweleko wa sasa wa uharibifu wa mazingira na tabianchi. Assumpta Massoi amezungumza na Dkt.

Sauti
4'8"
Picha: ILO

Kuwa mkimbizi sio tiketi ya umasikini

Mgahawa  wa kwanza wa wenye asili ya Syria wabisha hodi mjini Lisbon Ureno na kuwa kivutio.  Hii ni baada ya wakimbizi kutoka Syria waliopata hifadhi nchini humo kuamua kuenzi utamaduni na asili yao kwa kutumia mapishi yanayoeneza ladha ya chakula cha asili yao. Katika Makala ya leo Siraj Kalyango anaambatana na wakimbizi hao wakiwa katika mgahawa wao wakiandaa mapochocho yanayowakumbusha walikotoka lakini pia kuwaonjesha wenyeji wao ladha ya mila na utamaduni wa Syria kupitia mapishi, ungana naye.

 

Sauti
3'39"

Mkoa wa Morogoro waendeleza mapambano dhidi ya malaria

Leo ni maadhimisho ya siku ya malaria duniani yenye kauli mbiu” utayari wa kutokomeza malaria” .

Idhaa ya kiswahili kupitia mtangazaji wa redio washirika morning star ya Morogoro ,Pendo Thomas , ilibisha hodi Mkoani Morogoro  nchini Tanzania kujionea hali halisi ya tatizo la malaria.

 

Sauti
4'3"

Ukimtunza ngombe wako, maziwa hayakupigi chenga

Umoja wa Mataifa na mashirika wenza  wamekuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha wanawake vijijini katika programu za ujasiriamali kwa ushirikiano na serikali mbalimbali duniani kote.

Nchini Bangladesh Serikali  kwa ushirikiano na shirika la chakula na kilimo FAO wameendelea kuwasaidia wanawake wa vijijini kupitia miradi ya kilimo na ufugaji ili kuwawezesha kijikwamua na umaskini kama ilivyo katika agenda ya maendeleo enedelevu ya mwaka 2030.

Sauti
3'42"
UN Photo/Eskinder Debebe)

Winnie Mandela-shujaa aliyebeba mkuki kutetea wanyonge

Winnie Nomzamo  Madikizela Mandela! aliaga dunia mwezi huu wa Aprili! Daima atakumbukwa kwa harakati zake za ukombozi wa taifa la Afrika Kusini dhidi ya  ukatili wa ubaguzi wa rangi ulioshamiri nchini humo karne ya 20. Ma Winnie kama alivyojulikana zaidi licha ya taswira yake kukumbwa na misukosuko wakati wa uhai wake, kifo chake kiligeuka fursa kwa watu wengi kuweza kumfahamu zaidi na kujifunza tofauti na mengi maovu yaliyosemwa wakati wa uhai wake.

Sauti
3'58"
UN News/Selina Jerobon

Makabila Kenya sasa ni 44, ni baada ya wamakonde na wahindi nao kutambuliwa

Uhamiaji kwa sasa unakumbwa na madhila makubwa. Watu wanahama kwa sababu mbalimbali ikiwemo kusaka maisha bora, elimu, ajira, kuanzisha familia na nyingine nyingi. Nchini Kenya wahamiaji walitoka mbali hata bara hindi na nchi jirani kama vile Tanzania na Msumbiji. Kenya imechukua hatua kuunga mkono utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan lengo namba 10 la kutaka mienendo salama ya binadamu ikiwemo uhamiaji bora. Sasa wageni wanapata uraia nchini Kenya na kunufaika na huduma mbalimbali. Je nini kinafanyika?

Audio Duration
4'2"
UN/maktaba

Majuto mjukuu, kijana tambua ujana ni maji ya moto

Nchini Thailand kile kilichoonekana kuwa ni raha ya aina  yake kwa msichana mmoja baada ya kukutana na mpenzi wake kupitia mtandao wa kijamii, kimegeuka shubiri baada ya kujikuta na ujauzito bila kujua cha kufanya. Mtoto huyo wa kike aitwaye jina la Fang alikata tamaa ya maisha na kujilaumu kila uchao. Hata hivyo kupitia mradi wa makazi ya dharura unaoungwa mkono na shirika l aUmoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA mtoto Fang sasa ameweza kuona nuru kwenye maisha  yake. Je nini kimefanyika? Ungana basi na Assumpta Massoi kwenye makala hii.

Audio Duration
4'6"
Picha ya IFAD/Santiago Albert Pons

Wachuuza nyanya na mboga mboga ili kujinasua kutoka lindi la umaskini

Umoja wa Mataifa  na wadau wake unachagiza maendeleo ili kubadili maisha ya wakazi wa dunia hii ikiwemo kutokomeza umaskini. Na ndio maana chombo hicho kilipitisha malengo ya maendeleo endelevu,. SDGs ambapo lengo namba moja ni la kutokomeza umaskin ifikapo mwaka 2030. Ni kwa kuzingatia hilo wanawake wa wilaya ya Lwengo, Kusini mwa Uganda nao wameamua kujifunga kibwebwe kuweza kutokomeza umaskini.  Wameanzisha soko lao ambalo linauza bidhaa mbalimbali za matunda kama vile nyanya , na mboga za majani. Siraj Kalyango alivinjari eneo hilo na kukuandalia makala ifuatayo.

Sauti
3'32"
Picha: UNHCR/Video capture

Michezo yawa daraja la kuwanganisha vijana Somalia

Michezo na sanaa imekuwa daraja muhimu la kuwaunganisha wasomali hususan vijana ambao vita vya miaka nenda miaka rundi viliwakatisha tamaa ya mustakhbali wao. Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSOM kwa kutambua umuhimu wa michezo sio tu kwa kuwaleta watu pamoja bali katika mchakato wa kusaka amani , ukishirikiana na wizara ya michezo ya Somalia uliandaa mashindano ya riadha kwa vijana Somalia siku ya kimataifa ya michezo kwa ajili ya amani na maendeleo.

Sauti
3'48"

Bima ya afya ni muarobaini wa afya kwa wote- Dkt. Maro

Upatikanaji wa bima ya afya kwa kila mtu ni suala mtambuka  ambalo Umoja wa Mataifa na mashirika yake , wameendelea kulipigua chepuo ili ifikapo mwaka 2030 kila mtu bila kujali rika, uwezo au rangi yake ana uwezo wa  kununua bima ya afya. Utekelezaji wa hoja hiyo unaenda sambamba na mpango wa kimataifa wa kuhakikisha kila mtu anapata huduma ya afya popote pale alipo, UHC au Universal Health Coverage.

Sauti
4'1"