Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Mwaka 2018 umekuwa moto na wa moto

Matukio ya majanga yaliyoongezeka hivi karibuni  kama vile athari za mvua kubwa na pepo za Monsoon, na moto wa msituni ni ishara kwamba athari za mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri, kwa mujibu wa shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani-WMO.

 Katika taarifa yake ya hivi majuzi shirika hilo limethibisha kwamba   kiwango cha joto duniani kinaendelea kupanda  haraka zaidi na kusababisha athari nyingi ikiwemo misitu kukauka na kuwa hatarini ya kushika moto haraka. Kwa undani wa hali hiyo ungana na Siraj Kalyango katika makala hii.

Sauti
3'59"
Alhagie Manka/ UNFPA Gambia

Vijana wakishikwa watashikamana kuleta maendeleo katika jamii

Vijana ni nguzo muhimu ya kufanikisha ufanisi wa malengo ya maendeleo endelevu au SDGs kwa kuwa wana uwezo na  busara kuweza kuongoza dunia kesho na hata leo. Ili kutimiza hayo vijana hao wanapaswa kuwezeshwa leo kwa kupewa mafunzo yanayohitajika ,ikiwemo kupata elimu ya kutosha, kupata chakula, huduma za afya bora pamoja na malezi mazuri.

Audio Duration
4'
Picha: UM/Video capture

Ndoto zilizoingia katika mashaka ukimbzini, Uganda.

Vijana  ndio nguzo za kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, kwani ndio viongozi wa sasa na  wa hapo baadaye. Lakini wengi wanakabiliwa na  changamoto za kuweza kufanya vitu ambavyo vitawafaa hapo baadaye. Hali ya vijana katika mataifa yanayaoinukia ni ya shida mno. Hii ni kwa kuwa hujikuta ndoto zao za kujiendeleza wakati mwingine zinakwama kabisa na huenda si kwa sababu za kujitakia.

Sauti
3'45"
PICHA: UNHCR/Maktaba/Eduardo Soteras Jalil

Wanawake Burundi tumetoka mbali,japo bado kuna changamoto:Nzeyimana

Wanawake nchini Burundi wamepiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo masuala ya uongozi baada ya serikali kuwahakikishia uwakilishi wa asilimia 30 bungeni.

Hata hivyo bado kuna changamoto katika kutimiza malengo ya maendeleo  endelevu SDG’s yahusuyo wanawake kama usawa wa kijinsia, elimu, haki za kurithi na fursa za kiuchumi hususan wale waishio vijijini.

Sauti
4'27"
UNICEF/UN0201091/Herwig

Wakimbizi si maadui, ni watu wa kawaida waliokimbia kwao kutokana na taabu- Mariella

Shida inapobisha hodi mara nyingi binadamu hukata tamaa na kuamini kuwa huo ndio mwisho wa maisha  yake. Ingawa hiyo kwa wengine kukata tamaa ni mwiko kwa kuwa wanaamini kuwa mlango mmoja ukifungwa, mingine mingi hufunguka. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Mariela Shaker, mkimbizi kutoka Syria ambaye alipo hii leo, katu hakuna mtu ambaye angaliwaza kuwa angaliweza kufika. Vita, mateso, ghasia, ndio yalikuwa mazoea hadi siku ambayo anakwenda kuchukua diploma yake baada ya kuhitimu chuo, kombora likasambaratisha ndoto zote.

Sauti
4'13"
UN-Habitat/Julius Mwelu

Kenya tumeweka mikakati kabambe kuhakikisha tunafikia SDGs-Gituka

Wakati jukwaa la ngazi ya juu la kutathmini utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs likiendelea jijini New York, Marekani, Kenya imesema imeweka mipango kabambe kuhakikisha inafanikisha malengo hayo. Licha ya kwamba kuna changamoto lakini Kenya imeelezea kuoanisha  malengo katika wizara na kazi zingine za serikali kama moja ya mbinu za kuhakikisha malengo hayo yanasogezwa mbele.

Sauti
3'54"

Tunawapatia vijana stadi za kujikwamua kama kusuka nywele na ushoni- FPMHE

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mashirika ya kiraia yamekuwa yakiunga mkono harakati za kukwamua vijana kutoka katika madhila mbalimbali ikiwemo umaskini. Hatua hiyo inatokana na ukweli kwamba vita nchini humo vimesababisha vijana wa kike na wa kiume kujitumbukiza kwenye mambo yasiyofaa kama vile uasherati, uvutaji wa bangi na hata uporaji. Miongoni mwa mashirika hayo ni FPMHE ambao ni mfuko wa kidugu ulioasisiwa na mchungaji Maurice D’Hoore pamoja na Marceline Tawembi-Njdeka. Bi.

Audio Duration
4'5"