Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya migomba kupata mnyauko, wakulima Kagera wageukia Mihogo

Baada ya migomba kupata mnyauko, wakulima Kagera wageukia Mihogo

Pakua

Nchini Tanzania wakulima kwa kushirikiana na serikali na shirika la chakula na kilimo duniani, FAO wanatekeleza mbinu za kilimo bora kwa lengo la kuhakikisha siyo tu wanakidhi mahitaji ya  kila siku bali pia kuweza kuuza na pia kuhifadhi kwa siku za usoni.

 Mathalani mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa Tanzania wakulima baada ya kuona kilimo cha migomba kinakumbwa na magonjwa, baadhi wamegeukia sasa kilimo cha mihogo, na kutokana na mbinu za kisasa za kuhifadhi mazao, wanaweza kujipatia kipato na uhakika wa mlo. Je nini kinafanyika? shuhuda wetu ni Nicolaus Ngaiza, wa radio washirika Kasibante FM na ambaye amevinjari katika mashamba ya wakulima! 

Audio Credit
Nicholas Ngaiza
Audio Duration
4'24"
Photo Credit
Photo: David Monniaux