Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Hadithi simulizi zaimarisha elimu kwa kuleta ladha tofauti

Msemo wa mwacha mila ni mtumwa umedhihirika kufuatia mradi unaotekelezwa katika shule moja mkoani Morogoro nchini Tanzania ambako ajuza wanaopatiwa msaada katika kituo cha malezi ya wazee shuleni hapo wameajiriwa kusimulia hadithi kwa wanafunzi ambazo zinatoa elimu na mafunzo kuhusu masuala mbalimbali.

Mpango huo unarejea utamaduni wa kiafrika wa siku za nyuma ambapo mababu zetu walipitisha ujumbe au kutoa mafunzo kwa jamii kwa njia ya hadithi walizosimulia.

Sauti
4'22"

Nishati ya kupikia bado ni mtihani mkubwa kwa wanawake Ziwa Albert

Upatikanaji wa nishati ya kupikia ambayo ni moja ya mahitaji ya msingi bado unakabiliwa na changamoto wakati huu ambapo kuna mwamko kuhusu umuhimu wa kulinda mazingira na kutumia nishati mbadala.  

Mila na desturi katika jamii pia zinaonekana kuchangia katika kuongeza shinikizo zinazokabili wanawake katika kusaka kuni hususan maeneo ya vijijini ambako upatikanaji wa nishati mbadala ni ngumu.

Sauti
3'50"

Utimizaji wa SDGs unategemea juhudi za kutunza mazingira-WWF

Utunzaji wa mazingira ni suala jumuishi kwani linaathiri kila mtu. Nchini Kenya wenyeji wa kaunti ya Naivasha, kufuatia mafunzo waliyopokeana shirika la World Wide Fund for nature (WFF) wanatunza mazingira na wakati huo huo kuimarisha kipato chao kwani kilimo kinategemewa kwa nafasi kubwa.

Kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi juhudi za serikali, mashirika binafsi na jamii zinahitajika ili kufanikisha lengo la malengo ya maendeleo endelevu SDGs na malengo yote kwa jumla.

Sauti
3'47"
PICHA: Tanzaniakidstime/John Kabambala

Simulizi za hadithi zarejeshwa kwa watoto mkoani Morogoro nchini Tanzania

Katika mkoa wa Morogoro ulioko mashariki mwa Tanzania, shirika moja la kiraia limebuni mbinu za kuleta pamoja wazee na watoto kama njia mojawapo ya kuimarisha utamaduni na kuboresha stadi za maisha kwa watoto na vijana.

 Shirika hilo Childhood Development Organisation, CDO, limeanzisha mbinu huyo ambayo kwao wazee wanasimulia hadithi kwa watoto wenye umri wa kuanzia mwaka mmoja.

Sauti
3'19"
UN SDGs

Utoaji haki Uganda usiengue maskini

Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yameangazia masuala yote muhimu yanayogusa jamii yetu zama za sasa. Mathalani suala la watu kufurushwa kutoka kwenye nyumba zao au hata kufungwa kinyume cha sheria.

Lengo namba 16 limeangazia  masuala ya upatikanaji wa haki kisheria, ujenzi wa amani na uwepo wa  jamii jumuishi. Ni kwa mantiki hiyo John Kibego amefuatilia usakaji wa haki nchini Uganda katika masuala ya ardhi akizungumza na baadhi ya watu walionyimwa haki zao. Ungana naye  katika makalahii.

Sauti
3'32"

UNIC Tanzania yanoa wachora vibonzo ili waeneze haki za binadamu

Suala la haki za binadamu ni moja ya misingi ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mwaka 1945. Na ndio maana chombo hicho kilipitisha tamko la haki za binadamu lililo msingi wa katiba, kwa nchi zilizoridhia nyaraka hiyo ikiwemo zile za Afrika Mashariki. Hivi sasa kuelekea miaka 70 ya tamko hilo, Umoja wa Mataifa unatumia kila mbinu kueneza haki hizo na hasa inatumia vijana kuhakikisha kupitia stadi zao wanaelimisha jamii juu ya haki kama za kuishi, kujieleza, kula, kucheza, kutembea na kadha wa kadha.

Sauti
3'49"
Giles Clarke for UNOCHA

Makazi mapya yanayozingatia mazingira yaleta ahueni kwa wakimbizi wa Yemen

Yemen, nchi iliyogubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe zaidi ya miaka mitatu sasa. Mamia ya maelfu ya raia wamefurushwa makwao na sasa wanaishi ndani au nje ya nchi hiyo. Maisha ya ukimbizini ni magumu na yanakuwa magumu zaidi pale ambapo makazi ambayo unaishi hayahimili joto wala baridi. Jua linakuwa lako, halikadhalika mvua. Hali hiyo ndio imekumba wakimbizi wa Yemen waliosaka hifadhi kwenye moja ya majimbo  ya nchi hiyo.

Sauti
3'49"

Ukitaka kuwa mwandishi ni lazima usome kazi za waandishi wengine- Walibora

Sanaa ni chombo ambacho kinatumika sio tu kuburudisha lakini pia kupitisha ujumbe na wakati mwingine pia mafundisho. Mashairi ni moja ya kazi za sanaa ambazo kwa mujibu wa wataalam hutangulia fasihi au kazi yeyote ya riwaya. Katika makala hii yenye burudani si haba, Grace Kaneiya amezungumza na Ken Walibora ambaye ni mwandishi wa riwaya na mashairi kutoka nchini Kenya. Bwana Walibora ambaye anasema kwamba uandishi sio kitu ambacho aliwahi kufundishwa na mtu bali ni kipaji, anatoa ushauri kwa wale walio na ndoto ya kuwa waandishi.

Sauti
4'
UN News

Haki za watoto ni haki za binadamu lazima ziheshimiwe:UNICEF

Haki za watoto ni haki za binadamu na zinapaswa kuheshimiwa na kutekelezwa katika kila ngazi kuanzia kwenye familia, jamii na hata serikali kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Hata hivyo shirika hilo linasema mara nyingi hazitekelezwi hususan suala la ukatili, kuwatelekeza, mimba za utotoni  na hata kutowapa elimu. Nchini Tanzania serikali imelivalia njuga suala hilo likitaka kila kijiji, wilaya na mkoa kuchukua hatua kuhakikisha haki hizo zinatambuliwa na kuzingatiwa kwa kushirikisha wadau wote katika jamii wakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali.

Sauti
4'47"