Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Jiji la Dar es salaam lapendeza shukrani kwa UM

Ikiwa leo ni siku ya miji duniani, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imeangazia ni kwa jinsi gani chombo hiki chenye wanachama 193 kinasaidia nchi wanachama kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan lengo namba 11 la miji endelevu na jamii. Hatua hiyo inazingatia kwamba kasi ya ukuaji wa miji ni kubwa huku huduma za kijamii zikikua katika kasi ndogo.

Sauti
4'42"
PICHA: UNHCR/Maktaba/Eduardo Soteras Jalil

Ukiwa na kiongozi mvumilivu utakula mbivu:Jane Kamau

Kongamano la kimataifa la wanawake viongozi kutoka barani Afrika lilokuwa linafanyika mjini Bujumbura,Burundi limekunja jamvi kwa kuwahamasisha wanawake kujitokeza mstari wa mbele kuchangamkia  nyadhifa mbalimbali za uongozi nana mustakhbali wa mataifa yao. Hili ni moja ya malengo muhimu ya maendeleo endelevu SDG’s yanayochagiza mataifa kutoa fursa na kuwawezesha wanawake kama usawa wa kijinsia unaojumuisha kushika nafasi mbalimbali za maamuzi ifikapo mwaka 2030.

Sauti
4'43"
UN Photo/Lois Conner

Msanii mchoraji mwenye ulemavu wa macho.

Msanii Ritah Kivumbi anapenda sana tasnia ya sanaa ya uchoraji ingawa yeye ni ana ulemavu wa kutokuona. Alipata tatizo hilo alipokuwa mtu mzima. Baada ya kuona kuwa hawezi kuajiriwa tena, ari yake ya sanaa ya uchoraji iliongezeka ingawa anafanya hivyo kwa kupapasapapasa tu huku akichora michoro anayofikiria. Kama isemavyo kuwa ulemavu si kutokuwa na uwezo, Bi. Kivumbi ameweza kuendeleza kipaji chake na pia kujipatia pato kutokana na kazi yake hiyo licha ya ulemavu wake wa kutoona. Je anafanya nini? Kwa kina ungana basi na Siraj Kalyango katika makala hii.

Sauti
4'36"

Siku ya UN, wakimbizi Uganda wapaza sauti

Ikiwa leo ni siku ya Umoja wa Mataifa, makundi mbalimbali yamezungumzia kile ambacho chombo hicho kinawasaidia katika zama za sasa zilizogubikwa na changamoto lukuki. Umoja wa Mataifa wenye wanachama 193 unahakikisha kuwa rasilimali kidogo iliyopo inatumika kuleta maisha bora hata kwa watoto na vijana wakimbizi ambao kwao maisha ni machungu na hivyo wamekimbilia ugenini. Mfano ni nchini Uganda ambako katika siku hii ya Umoja wa Mataifa, John Kibego amevinjari na kuzungumza nao.

Sauti
3'23"
©FAO/Amos Gumulira

Mkulima kutoka Kagera asimulia FAO Tanzania ilivyomkomboa

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limeendelea na harakati zake za kusaidia nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinafanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan namba 1 la kutokomeza umaskini na lile la pili la kutokomeza njaa. Mfano huko  nchini Tanzania hususan mkoani Kagera FAO imefungua fursa kwa jamii kama vile wanawake kujikwamua kimapato kupitia kilimo. Fursa hiyo imedhihirika kwa mmoja wa wakulima ambaye ametembelewa na Nicolaus Ngaiza wa radio washirika Kasibante FM mkoani Kagera nchini Tanzania.

Sauti
3'51"
UN

Ethiopia yaazimia kuondokana na DDT, UNEP yaipatia msaada

DDT kemikali yenye sumu iliyolenga kuangamiza wadudu waharibifu wa mimea na hata wanaosambaza ugonjwa wa Malaria yaani mbu imebainikuwa pale inapotumika husalia ardhini na kuharibu siyo tu mazingira bali pia afya ya binadamu na Wanyama.

Tayari nchi nyingi zimepiga marufuku matumizi ya DDT ilhali zingine zikiona bado zina uwezo wa kuitumia bila madhara yoyote. Kwa zile ambazo zimeamua kuteketeza maelfu ya tani ya DDT, shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, limeamua kuzisaidia na miongoni mwao ni Ethiopia.

Sauti
3'41"
(Picha: Idhaa ya Kiswahili/Grace Kaneiya)

Sote tuwe wainjilisti wa dunia yenye mazingira bora- Rocky

Nyota ya mwanamuziki mashuhuru kutoka Ghana, Rocky Dawuni inazidi kung'ara  katika anga za kuchechemu dunia kutekeleza yale yaliyo bora kwa maslahi ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo. Mwanamuzi huyu ambaye amekuwa akitumia kipaji chake cha kuimba kupazia sauti masuala yanayoweka hatarini mustakabali wa binadamu, amezidi kuonekana na hata kuchaguliwa kuwa mwakilishi wa taasisi mbali mbali ikiwemo zile za Umoja wa Mataifa.

Sauti
2'47"

Wakulima tumenifaika na mradi wa FAO

Kwa msaada wa Muungano wa Ulaya, EU, Shirika la chakula na kilimo duniani FAO mwaka 2015 lilianzisha mafunzo ya kilimo bora kinachohifadhi mazingira kwa wakazi wa kaunti nane nchini Kenya. Lengo ni kuwasaidia wakulima hao kuongeza uzalishaji wa mazao na pia kuwaunganisha na masoko ya uhakika na  hatimaye kuweza kupunguza umaskini, kutokomeza njaa na hata kuboresha lishe ya familia.  Je nini kilifanyika? Grace Kaneiya anasimulia zaidi katika makala haya yaliyowezeshwa na FAO.

Sauti
2'15"

Umaskini bado ni changamoto kwa baadhi ya wananchi wa Burundi

Leo ikiwa ni siku ya kutokomeza umaskini duniani, ambalo ni lengo la kwanza la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs Umoja wa Mataifa unasema bado watu milioni 700 kote ulimwenguni wanaishi kwenye lindi la umaskini, bila kufahamu mlo wao wa kesho utatoka wapi, bila kuwa na uhakika pia wa kipato cha kuwezesha familia kukimu mahitaji mengine muhimu ya kila siku.

Sauti
4'1"