Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Semiyah Photography, 2017

Jamaica yafurahi muziki wake wa mtindo wa Reggae kutambuliwa na UNESCO

Muziki mbali na kuelimisha, kufahamisha, kuliwaza ama kuburudisha lakini pia kwa upande mwingine ni tunu inayotumika kutambulisha jamii ya eneo fulani kwa wakati fulani. Kupitia muziki, jamii kutoka upande mmoja inaweza kufahamu utambulisho wa mwingine na imefika wakati hata jamii moja kuiga tamaduni hiyo, mathalani muziki wa mtindo wa reggae kutoka Jamaica, ambao sasa umeenea kote duniani  hadi umetambuliwa na  shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni-UNESCO kama turathi za tamaduni zisizogusika za kibinadamu. Je ni kwa vipi?

Sauti
1'27"
Photo UNAMA / Abbas Naderi

Kubadili mifumo ndio muarobaini wa haki za huduma za jamii Tanzania: Dkt.Bisimba

Nchini Tanzania ingawa katika katiba  imeaainishwa haki za huduma za jamii kwa wote, mifumo iliyopo inafanya kuwa changamoto kubwa ya utekelezaji wa haki hizo. Hayo yamesemwa na Dkt.Helen Kijo Bisimba mwanaharakati wa muda mrefu wa haki za binadamu nchini humo. Akijadili ibara ya 21 ya tamko la haki za binadamu  isemayo “kila mtu ana haki ya kushiriki katika serikali yake, haki sawa za huduma za jamii ikiwa ni pamoja na serikali kuongoza kwa matakwa ya wananchi”, Dkt.

Sauti
5'29"

Katu mtu asilazimishwe kujiunga na chama hata ndani ya familia- Wakili Komba

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka  huu linatimiza miaka 70 tangu kuasisiwa lina ibara 30 ambazo ni msingi wa haki za binadamu kote duniani. Licha ya kuwepo kwa muda mrefu baadhi ya haki zinasiginwa katika baadhi ya maeneo na sababu kuu ni kwa wanachi kutofahamu vyema haki zao. Ni kwa msingi tumekuwa tunakuletea uchambuzi wa Ibara kwa Ibara ambapo leo Wakili Aloyce Komba kutoka Tanzania amezungumza na Arnold Kayanda wa Idhaa hii akifafanua ibara ya 20.

Sauti
4'18"
Picha na UN News/Yasmina Guerda

Anasemekana kuwa mwanamke wa kwanza wa kanda ya Afrika mashariki na kati kupata shahada ya Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza mwaka wa 1954.

Wakati  harakati za siku 16 za kuhamasisha kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake zikiwa zinaendelea, leo tuko nchini Uganda kusikia mchango wa mama mmoja ambae sasa ni marehemu lakini alikuwa mpigania haki za wanawake nchini humo. Dkt Sarah NYENDWOHA Ntiro ambae anasemekana kuwa mwanamke wa kwanza kanda ya Afrika mashariki na kati kupata shahada ya Chuo Kikuu kutoka Chuo Kikuu  cha Oxford nchini Uingereza mwaka wa 1954 katika somo la Historia.

Sauti
3'12"
IOM/Amanda Nero

Nuru yaonekana katika juhudi za kulinda maeneo oevu, Uganda

Ulinzi wa mazingira umekuwa ukipigiwa upatu na Umoja wa Mataifa kama moja wa juhudi za kuona dunia yetu haihatarishwi na majanga yatokanayo  na uharibifu wa mazingira. Mito ni moja wa sehemu ambazo zinasadia maisha ya viumbe wengi kama mwanadamu na mifugo kwa kupata maji ya kunywa pamoja na matumizi mengine mengi.

Lakini  baadhi ya mito imekuwa ikichafuliwa huenda  kwa kutojua.Moja wa mito hiyo ni ule wa Kanywakono wilya ya Hoima , magharibi mwa Uganda.Kwa kuelewa zaidi hali huko ungana na mwandishi wetu John Kibego alifika huko na kutuandalia Makala ifuatayo.

Sauti
3'47"
©UNHCR/O. Akindipe

Baadhi ya watu hunyimwa haki yao ya kumiliki mali

Katika mwendelezo wa kupitia ibara za tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka huu wa 2018 linatimiza miaka 70, leo inamulikwa ibara ya 17 inayozungumzia haki ya mtu kumiliki mali yeye mwenyewe au kwa ushirika na mtu mwingine au wengine. Ibara hii inazingatia ukweli kwamba baadhi ya watu wananyimwa haki hiyo kwa misingi mbalimbali ikiwemo rangi, jinsia, kabila, dini au umri. Katika basi kuangazia utekelezaji wa ibara hiyo tunajikita katika mtu kunyimwa haki hiyo kwa misingi ya kijinsia na kutufafanulia hayo ungana na Siraj Kalyango katika makala hii.

Sauti
3'17"

Jinamizi la kutosajiliwa utotoni, laandama maelfu ya watu wasio na utaifa

Ibara ya 15 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linasisitiza haki ya mtu kuwa na utaifa. Iwe ni utaifa kwa kuzaliwa au kwa kusajiliwa katika nchi nyingine. Hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali zaidi ya watu milioni 12 hivi sasa duniani  hawana utaifa. Ukosefu wa utaifa  unapoka watoto na watu wazima haki zao za msingi. Je ni sababu gani basi zinafanya watu wakose utaifa, na ni madhila yapi basi wanapitia? Ungana basi na Grace Kaneiya katika makala hii.

Sauti
3'11"
UNIC Mexico/Antonio Nieto

Inahitaji utashi wa serikali kutekeleza ibara za haki za binadamu

Ibara ya 14 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa  inaeleza kuwa kila mtu ana haki ya kusaka na kuomba hifadhi katika nchi nyingine ikiwa anateswa nchini mwake.Katika mazungumzo na Arnold Kayanda, Mwanasheria, Wakili wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania, Jones Sendodo anasema inahitaji utashi wa serikali zilizoko madarakani kutekeleza ibara hizi kwani kuna hata nchi ambazo pamoja na kuridhia sheria na kanuni zinazowataka kutekeleza haki za binadamu, bado hazifanyi hivyo.

Sauti
3'2"
UN/Elma Okic Edit

Je wajua maana ya haki ya faragha kwa mujibu wa tamko la haki za binadamu?

Mtu ana  haki ya kuwa na faragha katika maisha yake na hii ni kwa mujibu wa ibara ya 12 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Neno faragha lina maana pana zaidi ambapo katika uchambuzi wa Ibara kwa Ibara za tamko hilo kwenye kuelekea kilele cha  miaka 70 ya tamko hilo, leo Siraj Kalyango amezungumza na mtaalamu wa sheria kutoka Tanzania ili uelewe zaidi.

Audio Duration
2'50"
UNICEF/Seck

Asante Tanzania lakini nyumbani ni nyumbani:Wakimbizi wa Burundi


Maelfu ya wakimbizi wa Burundi wanaopata hifadhi nchini Tanzania wanaendelea kurejea nchini mwao kwa msaada wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR kufutia makubaliano maalum kati ya serikali ya Burundi na ya Tanzania yaliyofikiwa yaliyoafikiwa katika mwezi Machi mwaka huu. Kufikia sasa inakisiwa wakimbizi takriban elf 72 watakuwa wamerejea Burundi kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Wakimbizi wapatao elf mbili wanaondoka kila wiki kwenye kambi tatu zilizoko magharibi mwa Tanzania na kurudi Burundi

Sauti
4'26"