Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Picha: UM/Video capture

Muziki wa kizazi kipya ndio unauza siku hizi.

Muziki ni kifaa muhimu kinacholeta mabadiliko katika jamii.Muziki unaweza ukawafikia mamilioni ya watu,na kwa kuhamasisha jamii kuhusu changamoto za kijamii, kiuchumi na kimazingira ambavyo ndivyo msingi wa maendeleo endelevu SDGs.

Sauti
5'41"

Ukatili dhidi ya wanawake ni adui ya SDGs

Wanawake na wasichana, popote pale wanahitaji kuwa na haki na fursa sawa na pia wawe huru kuishi katika mazingira yasiokuwa na ukatili wala ubaguzi. Usawa wa jinsia na uwezeshaji ni lengo namba tano la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na ni muhimu katika kufikia maendeleo hayo kama yalivyoainishwa na Umoja wa Mataifa. Hata hivyo ukatili majumbani ni moja ya changamoto zinazokwamisha kufikia usawa huo wa jinsia. Je nchini Uganda hali ikoje mwandishi wetu John Kibego anatupeleka moja kwa moja hadi wilaya ya Hoima nchini humo. Ungana naye.

Sauti
3'32"
Piacha ya UNICEF/Narendra Shrestha

Baa la njaa lasababisha wanavijiji kukimbia makwao

Tatizo la mabadiliko ya tabianchi ni kikwazo kikubwa kwa wanawake viijijini ambako ukosefu wa mvua na ukame vinakwamisha uzalishaji wa mazao, hivyo kufanya maisha kuwa magumu kwa siyo tu kwa wanawake hao bali pia jamii ambazo zinawategemea.

Je ni kwa vipi athari hizo ni mwiba kwa wanawake? Fuatana nami basi Patrick Newman hadi nchini Nepal ambako mabadiliko ya tabianchi yameleta  baa la njaa  katika baadhi ya vijiji na kusababisha baadhi ya wananchi kuhamia nchi za nje, kutafuta maisha bora

Sauti
3'36"

Muziki wetu ndio uchawi pekee, ukiwa na shida, unaondoa mawazo

Kila kabila barani Afrika lina utamaduni wake, na kila utamaduni huambana na ngoma za asili. leo katika makala yetu tunaelekea magharibi mwa  Uganda kando mwa ziwa Albert ambako mwandishi wetu John Kibego alishuhudia miondoko ya ngoma za asili za watu wa kabila la wagungu.

Wenyewe wanadai ngoma zao sio burudani tu kama tulivyozoea bali  huambatana na mafundisho, burudani na elimu kwa vijana wanaochipukia. Unagana nasi  katika makala hii upate undani zaidi.

Sauti
3'31"

Malengo ya maendeleo endelevu yana faida gani kwa jamii ya Afrika?

Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika ya kibinadamu wako katika kampeni madhubuti wakipigia  chepuo agenda ya malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030. Kapeni hiyo inayozijumuisha serikali mbalimbali duniani, ni moja ya njia sahihi ya kuleta usawa na maendeleo kwa nchi masikini kwa mfano upigaji vita uharibifu wa mazingiza, kupigania usawa kijinsia, afya bora na ajira zikiwa ni baadhi tu ya malengo andelevu 17 za Umoja wa Mataifa.

Sauti
3'34"
Picha: UNFPA/Omar Gharzeddine

Mtaala wa ujasiriamali wawezesha wanafunzi Msumbiji kujikimu

Barani Afrika idadi ya vijana kama ilivyo katika mabara mengine inaongezeka kila uchao. Kasi ya ongezeko hilo haiendi sambamba na mabadiliko ya stadi shuleni ili waweze kupata ujuzi wa kuwawezesha kukabiliana na maisha yao. Ni kwa kuzingatia hilo, Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la maendeleo ya viwanda, UNIDO limeanzisha mradi wa kujumuisha mtaala wa ujasiriamali katika shule za msingi na sekondari barani Afrika.

Sauti
3'30"

Maisha ya kambini ni magumu ila tunapambana : Johari Nanangu

Migogoro ya kivita katika nchi za  maziwa makuu, zina aathiri maisha ya mamilioni ya raia wasio na hatia, ambapo wengi wao ni wanawanke na watoto.

Nchini Burundi mwandishi wetu wa maziwa makuu, Ramadhani kibuga alitembelea kambi wa wakimizi  ya kavumu, ambako  amezungumza na mwanamke jasiri ambaye, licha ya matatizo ya kila siku ya kambini  bado anafanya shughuli za ujasiriamali ili kujikwamua kimaisha.

Biashara gani anafanya na je anafaidika vip? Ungana na Kibuga   katika makala hii upate undani zaidi.

Sauti
3'50"