Fanya kazi kwa bidhii utafanikiwa, acha kuwinda watu wenye ulemavu wa ngozi
Imani potofu kwa baadhi ya watu ya kwamba watatajirika iwapo watapeleka viungo vya mtu mwenye ulemavu wa ngozi kwa waganga wa kienyeji imekuwa ikikatili maisha ya binadamu hao na kuwaacha wengine na madhara makubwa ya kisaikolojia na kimwili katika maisha yao yote, wakati vitendo hivyo vikiendelea katika jamii, hususan ya waafrika waishio kusini mwa jangwa la sahara.
Umoja wa Mataifa na wadau wamekuwa wakihimiza serikali, asasi za kiraia na jamiikuondokana na imani hizo potofu na kuthamini maisha ya kila mtu.