Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN Photo/Rick Bajornas)

Mbele ya sheria watu wote bila kujali rangi, umri au maumbile ni sawa na wanastahili haki sawa

Takriban miaka 70  imepita tangu  tamko la haki za binadamu litolewe. Tamko hilo lina ibara 30 lakini leo tunaangazia ibara ya SABA.  Ibara hiyo inasema kuwa “Mbele ya sheria watu wote ni sawa na wanastahili haki sawa za kulindwa. Ili kupata uelewa zaidi wa ibara hiyo Siraj Kalyango wa idhaa hii amezungumza na  mwanasheria kutoka Tanzania ambaye anaanza kwa kujitambulisha.

Sauti
3'54"
UN Photo/Emmanuel Hungrecker

Mara nyingi haki za watu wengi hubinywa kutokana na sababu kama vile, vita, mfumo wa utawala na hata mgawanyiko katika jamii.

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Ibara ya 6 inasema kila mtu anayo haki, binafsi au kwa ushirikiano na wengine, kuanzisha na kujadili dhana na kanuni mpya za haki za binadamu na kuzitetea ili zikubalike.” Lakini mara nyingi watu hawapati fursa ya kufanya hivyo na hata wakiiipata haki hizo hubinywa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo, vita, mfumo wa utawala na hata mgawanyiko katika jamii.

Sauti
4'31"
UN Photo - Jean-Marc Ferre

Mfuko wa kusaidia manusura wa utesaji waleta nuru kwa jamii

Ibara ya 5 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linalotimiza miaka 70 mwaka huu wa 2018, inaweka bayana kuwa hakuna mtu yeyote anayepaswa kuteswa kwa sababu yoyote ile. Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimetia saini na kuridhia tamko hilo lakini bado baadhi zinatuhumiwa kutesa watu kwa sababu mbalimbali jambo linaloleta ulemavu, madhara ya kisaikolojia na hata wengine hujiua. Je ni kwa kiasi gani madhila hayo yanakumba watu? Na huwa wanajisikia vipi wakati wa mateso na hata baada ya mateso? Jamii zao je?

Sauti
3'33"

Nchi zinatakiwa kubadili sheria zao ili kwenda sawa na mbinu za sasa za utumwa na utwana.

Ibara ya 4 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linalotimiza miaka 70 mwaka huu wa 2018, inaeleza kinagaubaga kuwa hakuna mtu anayestahili kugeuzwa mtumwa na wala kuwa mtwana wa mtu yeyote. Na ingawa kwa miaka mingi nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeridhia na pia kutunga sheria za kuunga mkono ibara hii, mabadiliko ya namna utumwa na utwana unavyotafsiriwa yaneziacha nyuma sheria nyingi. Wakili Jebra Kambole wa Tanzania katika mazungumzo haya na Arnold Kayanda, anasema kuna haja ya jumuiya ya kimataifa kulitizamasuala hili kwa namna mpya.

Sauti
2'51"
UN Photo.

Hukumu ya kifo sio dawa ya uhalifu- Bwana Ouko

Ibara ya tatu ya  haki za bindamu inasema kuwa kila mtu ana haki ya kuishi, haki ya kuwa huru na kulindwa. Lakini  mara nyingine haki hii hukiukwa kwa sababu mbali mbali.

Na endapo hukumu ya kifo ikitekelezwa basi husababisha mtu kunyimwa haki hii iliyoorodheshwa katika tamko la haki za binadamu.

Sauti
3'46"
World Bank/Dominic Chavez

Baadhi ya watu wanaozaliwa na hali ya kutoweza kujifunza Uganda hukosa haki zao

Katika mfululizo wa uchambuzi wa ibara za Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa leo tunaangazia ibara ya 2. Ibara hii inasema kwamba 

“Kila mtu anastahili kuwa na haki zote na uhuru wote ambao umeelezwa katika tamko hili bila ubaguzi wa aina yoyote kama vile rangi, taifa,jinsia, lugha,,dini,siasa,fikra,asili ya taifa la mtu,miliki, kuzaliwa au kwa hali nyingine yoyote.

Sauti
4'9"
UN Photo.

Tanzania bado kuna changamoto ya utekelezaji wa haki za binadamu

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mwezi disemba mwaka huu wa 2018 linatimiza miaka 70. Tamko hilo ni msingi wa haki za binadamu ulimwenguni kote na lilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1948. Kuelekea maadhimisho hayo leo tunaangazia Ibara ya kwanza ya tamko hilo lenye ibara 30 ambayo inasema“Watu wote wamezaliwa huru hadhi na haki zao ni sawa  wote wana akili  na wana dhamiri hivyo yapaswa watendeane kindugu” Lakini je ibara hii inatekelezwa ipasavyo?

Sauti
4'9"

Jiji la Dar es salaam lapendeza shukrani kwa UM

Ikiwa leo ni siku ya miji duniani, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imeangazia ni kwa jinsi gani chombo hiki chenye wanachama 193 kinasaidia nchi wanachama kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan lengo namba 11 la miji endelevu na jamii. Hatua hiyo inazingatia kwamba kasi ya ukuaji wa miji ni kubwa huku huduma za kijamii zikikua katika kasi ndogo.

Sauti
4'42"
PICHA: UNHCR/Maktaba/Eduardo Soteras Jalil

Ukiwa na kiongozi mvumilivu utakula mbivu:Jane Kamau

Kongamano la kimataifa la wanawake viongozi kutoka barani Afrika lilokuwa linafanyika mjini Bujumbura,Burundi limekunja jamvi kwa kuwahamasisha wanawake kujitokeza mstari wa mbele kuchangamkia  nyadhifa mbalimbali za uongozi nana mustakhbali wa mataifa yao. Hili ni moja ya malengo muhimu ya maendeleo endelevu SDG’s yanayochagiza mataifa kutoa fursa na kuwawezesha wanawake kama usawa wa kijinsia unaojumuisha kushika nafasi mbalimbali za maamuzi ifikapo mwaka 2030.

Sauti
4'43"
UN Photo/Lois Conner

Msanii mchoraji mwenye ulemavu wa macho.

Msanii Ritah Kivumbi anapenda sana tasnia ya sanaa ya uchoraji ingawa yeye ni ana ulemavu wa kutokuona. Alipata tatizo hilo alipokuwa mtu mzima. Baada ya kuona kuwa hawezi kuajiriwa tena, ari yake ya sanaa ya uchoraji iliongezeka ingawa anafanya hivyo kwa kupapasapapasa tu huku akichora michoro anayofikiria. Kama isemavyo kuwa ulemavu si kutokuwa na uwezo, Bi. Kivumbi ameweza kuendeleza kipaji chake na pia kujipatia pato kutokana na kazi yake hiyo licha ya ulemavu wake wa kutoona. Je anafanya nini? Kwa kina ungana basi na Siraj Kalyango katika makala hii.

Sauti
4'36"