Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jiji la Dar es salaam lapendeza shukrani kwa UM

Jiji la Dar es salaam lapendeza shukrani kwa UM

Pakua

Ikiwa leo ni siku ya miji duniani, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imeangazia ni kwa jinsi gani chombo hiki chenye wanachama 193 kinasaidia nchi wanachama kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan lengo namba 11 la miji endelevu na jamii. Hatua hiyo inazingatia kwamba kasi ya ukuaji wa miji ni kubwa huku huduma za kijamii zikikua katika kasi ndogo.

Hii ina maana kwamba wakazi wa miji wanakabiliwa na changamoto wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku, usafiri unakuwa wa shida, huduma za maji safi na majitaka halikadhalika. Hata hivyo sasa Dar es salaam, mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania unabadilika sura yake. Mwandishi Antony Joseph wa Radio Washirika Uhuru FM amevinjari na kuzungumza na wakazi pamoja na Dkt Hante Mukuki, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Audio Credit
Siraj Kalyango/Antony Joseph
Audio Duration
4'42"
Photo Credit
Ujenzi na usafiri ni miongoni mwa sekta zilizobeba ukuaji wa uchumi nchini Tanzania. Hapa ni mjini Dar es Salaam. Picha ya IMF.