Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

UN/Eskinder Debebe

Vijana tumieni mitandao ya kijamii kusaka fursa na si kufuatilia watu- Marygoreth

“Vijana waache kutumia muda wao mwingi kufuatilia habari za watu maarufu mitandaoni bali watafute fursa za kuwanufaisha wao na jamii zao.”Ni maneno ya Marygoreth Richard mwandisih wa habari wa  Media Action ya shirika la utangazaji la Uingereza,  BBC ambaye  alishinda tuzo ya  kushiriki programu ya mwaka huu ya Reham Al Farah Memorial inayowanoa waandishi wa habari kuhusu masuala ya Umoja wa Mataifa.

 

Sauti
3'33"
UN Photo/Herve Serefio

Wanafunzi Hoima wapaza sauti dhidi ya ukatili wa kijinsia

Hatimaye siku 16 za kupiga vita na kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa mwaka huu wa 2018 zimefikia tamati ambapo maeneo mbalimbali duniani yametamatisha kampeni hiyo kwa matukio tofauti. Mathalani huko nchini Uganda kwenye makazi ya wakimbizi wa Kyangwali mjini Hoima Magharibi mwa Uganda, wanafunzi walishiriki kwenye kilele cha maadhimisho hayowakielezea aina ya visa vya ukatili, wanaotekeleza na kile ambacho kinapaswa kufanyika, kama anavyosimulia mwandishi wetu nchini humo John Kibego aliyehudhuria shamrashamra hizo.

Sauti
3'38"
Ifad/Reproduction

Wakulima Bolivia waanza kufuata utaalam wa kijadi kuhusu mabadiliko ya tabianchi

Wakati viongozi wa ndunia wakiendelea kukuna vichwa mjini Katowice nchini Poland kusaka dawa mujarabu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwenye mkutano wa COP24 hadi Disemba 14, jinamizi hilo limeendelea kuziathiri jamii mbalimbali duniani.  Nchini Bolivia, takriban asilimia 40 ya watu wake wameathirika na mabadiliko ya tabianchi. Ukame  wa kila mara,  mafuriko, na theluji  vinaharibu mimea na kutishia uhakika wa chakula na mustakabali wa watu hao.

Sauti
3'17"
UN/Eskinder Debebe

Utamaduni wa jamii yako ni haki  yako, lasema tamko la haki za binadamu la UN

Katika mwendelezo wa uchambuzi wa ibara kwa ibara za tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa leo tunamulika ibara ya 27 inayosema kuwa kila mtu ana haki ya kushiriki na kunufaika na tamaduni, sanaa na sayansi ya jamii yake. Hii imenyumbuliwa katika pande mbili ambapo ili kuweza kupata ufafanuzi wa kisheria Grace Kaneiya wa Idhaa hii amezungumza na Dkt. Elifuraha Laltaika, mhadhiri wa sheria kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira nchini Tanzania na anaanza kwa kufafanua yaliyomo.

 

Sauti
2'2"
UNICEF/UN0153963/Obadi

Mkimbizi bila elimu ni sawa na mti bila matunda:Mkimbizi Rachel

Elimu kwa mkimbizi ni muhimu sana, kwani bila elimu huwezi fanya chochote , iwe ni kwa upande wa ajira au hata ujasiriliamali, unakuwa sawa na mti usiozaa matunda ambao huonekana kutokuwa na faida yoyote. Kauli hiyo ni ya mmoja wa wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidekrasia ya Congo DRC, ambaye aliishi na kusomea kambini nchini Uganda. Akizungumza na mwandishi wetu John Kibego kuhusu haki ya kila mtu kupata elimu bila kujali kabila, rangi au uraia wake kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya 26 ya tamko la haki za binadamu, anasema haijalishi mazingira uliyopo “elimu ni elimu”.

Sauti
3'32"
FAO/Giulio Napolitano

Ibara ya 24

Mapumziko na burudani ikiwemo kuwa na muda wenye ukomo wa kufanya kazi na pia kupatiwa likizo yenye malipo ni haki ya kila mtu kwa mujibu wa  Ibara ya 24 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linalotimiza miaka 70 mwezi huu. Lakini je haki hii ya msingi inatekelezwa vipi? Katika makala hii, Mwanasheria Tito Magoti wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Tanzania akijadili na Arnold Kayanda anaanza kwa kueleza mantiki ya ibara yenyewe.

 

Sauti
2'11"
UN Picha/Greg Kinch

Hali ya baadhi ya wafanyakazi ughaibuni inasikitisha- Emma Mbura

Ibara ya 23 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa inasema kila mtu ana haki ya kufanya kazi, kuchagua kazi anayoifanya, kufanya kazi katika mazingira salama na ulinzi dhidi ya ukosefu wa ajira. Kipengele cha pili kwenye ibara hiyo kinasema kuwa kila mtu, bila kubaguliwa ana haki ya kulipwa mshahara sawa kwa kazi sawa. Ibara hiyo inakwenda mbali zaidi na kusema kuwa kila mtu ana haki ya ujira unaofaa kwa ajili ya matumizi yake na familia kuwawezesha kuishi kwa utu na nyongeza kwa ajili ya ulinzi wa kijamii.

Sauti
5'14"
Semiyah Photography, 2017

Jamaica yafurahi muziki wake wa mtindo wa Reggae kutambuliwa na UNESCO

Muziki mbali na kuelimisha, kufahamisha, kuliwaza ama kuburudisha lakini pia kwa upande mwingine ni tunu inayotumika kutambulisha jamii ya eneo fulani kwa wakati fulani. Kupitia muziki, jamii kutoka upande mmoja inaweza kufahamu utambulisho wa mwingine na imefika wakati hata jamii moja kuiga tamaduni hiyo, mathalani muziki wa mtindo wa reggae kutoka Jamaica, ambao sasa umeenea kote duniani  hadi umetambuliwa na  shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni-UNESCO kama turathi za tamaduni zisizogusika za kibinadamu. Je ni kwa vipi?

Sauti
1'27"
Photo UNAMA / Abbas Naderi

Kubadili mifumo ndio muarobaini wa haki za huduma za jamii Tanzania: Dkt.Bisimba

Nchini Tanzania ingawa katika katiba  imeaainishwa haki za huduma za jamii kwa wote, mifumo iliyopo inafanya kuwa changamoto kubwa ya utekelezaji wa haki hizo. Hayo yamesemwa na Dkt.Helen Kijo Bisimba mwanaharakati wa muda mrefu wa haki za binadamu nchini humo. Akijadili ibara ya 21 ya tamko la haki za binadamu  isemayo “kila mtu ana haki ya kushiriki katika serikali yake, haki sawa za huduma za jamii ikiwa ni pamoja na serikali kuongoza kwa matakwa ya wananchi”, Dkt.

Sauti
5'29"

Katu mtu asilazimishwe kujiunga na chama hata ndani ya familia- Wakili Komba

Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka  huu linatimiza miaka 70 tangu kuasisiwa lina ibara 30 ambazo ni msingi wa haki za binadamu kote duniani. Licha ya kuwepo kwa muda mrefu baadhi ya haki zinasiginwa katika baadhi ya maeneo na sababu kuu ni kwa wanachi kutofahamu vyema haki zao. Ni kwa msingi tumekuwa tunakuletea uchambuzi wa Ibara kwa Ibara ambapo leo Wakili Aloyce Komba kutoka Tanzania amezungumza na Arnold Kayanda wa Idhaa hii akifafanua ibara ya 20.

Sauti
4'18"