Katu mtu asilazimishwe kujiunga na chama hata ndani ya familia- Wakili Komba
Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka huu linatimiza miaka 70 tangu kuasisiwa lina ibara 30 ambazo ni msingi wa haki za binadamu kote duniani. Licha ya kuwepo kwa muda mrefu baadhi ya haki zinasiginwa katika baadhi ya maeneo na sababu kuu ni kwa wanachi kutofahamu vyema haki zao. Ni kwa msingi tumekuwa tunakuletea uchambuzi wa Ibara kwa Ibara ambapo leo Wakili Aloyce Komba kutoka Tanzania amezungumza na Arnold Kayanda wa Idhaa hii akifafanua ibara ya 20. Ibara hii ina sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza inasema kila mtu ana haki na uhuru wa kukusanyika na kujiunga na kikundi ilhali sehemu ya pili inasema hakuna mtu anayepashwa kulazimishwa kujiunga na kikundi chochote. Wakili Komba anaanza kwa kufafanua kwa muhtasari ibara ina maana gani.