Wakimbizi Iraq wahangaika kujiandaa kwa majira ya baridi kali
Juhudi zinaendelea sasa nchini Syria, Iraq na nchi jirani, kuwaandaa wakimbizi wa kigeni na wa ndani kwa msimu wa baridi.
Juhudi zinaendelea sasa nchini Syria, Iraq na nchi jirani, kuwaandaa wakimbizi wa kigeni na wa ndani kwa msimu wa baridi.
Kongamano la kimataifa kuhusu usalama na ubora wa chakula linaendelea kwenye makao makuu ya Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA, mjini Vienna, Austria.
Mjadala wa uwiano kati ya mabadiliko ya tabia nchi, usalama wa chakula, kilimo na biashara umefanyika mjini Bujumbura Burundi ukiwaleta pamoja wataalamu wa sekta hizo kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wanadiplomasia na watunga sera.
Kutokomeza ajira kwa watoto ni jambo linalopigiwa chepuo kila uchao kutokana na kitendo hicho kutishia mustakhbali wao. Watoto wanapoajiriwa, haki zao kuu nne za msingi zinakuwa mashakani.
Wakati nchi ya Uganda ikiwa ni miongoni mwa nchi ambazo zinaubeba mzigo wa kuhifadhi wakimbizi barani Afrika Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) amefanya ziara nchini humo ili kutathmini hali halisi ya wakimbizi kambini na kubaini mbinu za kuima
Nchini Somalia, mzozo wa zaidi ya miongo miwili sasa umesababisha maelfu ya wakazi kusaka hifadhi ukimbizini. Walikosaka hifadhi ni pamoja na nchini Kenya kwenye kambi ya Dadaab ambako baadhi ya madhila ni kizazi hadi kizazi kuendelea kuongezeka bila kuwa na haki ya msingi ya utaifa.
Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa mapambano dhidi ya Ebola UNMEER, Anthony Banbury ametembelea manusura wa homa ya Ebola nchini Sierra Leone.
Pia ametumia fursa ya ziara hiyo kutembelea makaburi ya watu waliokufa kufuatia ugonjwa huo hatari unaoshamiri Afrika Magharibi.
Shirika la umoja wa mataifa wa Maendeleo na Kilimo (IFAD) kwa kushirikiana na serikali ya Rwanda imeanzisha mfumo uitwao "FlexiBiogas" ambayo ni mbinu ya kunasa gesi ya methane kutoka kinyesi cha ng'ombe ili kujenga mtambo wa gesi safi. Kutumia biogas kama nishati ni njia mojawapot ya
Urithi wa picha na sauti zitokanazo na matukio mbali mbali duniani uko hatarini!
Ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na baadhi ya viongozi wa dunia katika nchi za pembe ya Afrika imefufua matumini kiuchumi, kijamii na hata katika usalama.