Mambo mseto:mjadala mkuu tabianchi, jamii za asili vyamulikwaa
Kwa wiki nzima, Kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kimekuwa kinaendelea na mikutano yake hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Kwa wiki nzima, Kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kimekuwa kinaendelea na mikutano yake hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
Mjadala Mkuu wa mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ulioanza tarehe 24 Septemba mwaka 2014 umetoa fursa kwa viongozi wa nchi na serikali kuhutubia na kuelezea mambo muhimu ya kitaifa na kimataifa yanayohusiana na utekelezaji wa misingi ya Umoja wa Mataifa ambayo ni pamoja na ama
Katika kikao cha 27 cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea mjini Geneva, Mtalaamu Huru kuhusu Haki za Binadamu nchini Somalia, Bahame Tom Nyanduga, ametoa ripoti yake ya kwanza, akisisitiza changamoto zinazoikumba nchi hiyo.
Katika mjadala wa wazi wa kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amezungumzia jinsi bara la Afrika limeanza kuibuka baada ya kudhoofika kwa kipindi cha miaka mia tano ya ukoloni.
Nchini Rwanda juhudi za kibinafsi pamoja na utashi wa kisiasa zimechangia katika kupambana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi.
Tarehe 25 mwezi huu wa Septemba, Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa itazindua chapicho kuhusu adhabu ya Kifo. Tukio hilo litafanyika wakati ambapo Umoja wa Mataifa umekuwa unapigia chepuo kutokomezwa kwa adhabu hiyo.
Katika juhudi za kuimarisha maisha ya wakazi wa mkoani Mara nchini Tanzania benki ya dunia imefanya mradi wa kutoa mafunzo kwa ajili ya kuimarisha kilimo hususan ufugaji.
Katika kuboresha kilimo kinachohifadhi mazingira na kupunguza umasikini mpango maalum unaodhaminiwa na benki ya dunia umejikita katika nchi za Afrika Mashariki ili kuwezesha wakulima wadogowadogo kwa kuwapatia mafunzo na rasilimali.
Wakati Umoja wa Mataifa ukiendelea na maandalizi ya mkutano wa viongozi kuhusu mabadiliko ya tabianchi, tathmini iliyofanyika inaonyesha mafanikio yamepatikana katika kufikia lengo namba saba la malengo ya maendeleo ya milenia ambalo ni kuhakikisha uendelevu wa mazingira.
Wiki iliyopita mjini New York, ziliandaliwa shughuli mbili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kama sehemu ya kuadhimisha miaka 20 ya mradi wa kumbukumbu ya barabara ya biashara ya utumwa.