Kwenye siku ya urafiki Ban atoa wito watu watafute urafiki wa kweli
Julai 30 ni Siku ya Urafiki Duniani- na kulingana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, siku hiyo inakuja wakati vita, machafuko na kutoaminiana vimetanda kote duniani.
Julai 30 ni Siku ya Urafiki Duniani- na kulingana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, siku hiyo inakuja wakati vita, machafuko na kutoaminiana vimetanda kote duniani.
Lengo namba moja katika malengo manane yaliyowekwa na viongozi wa dunia mnamo mwaka 2000, ni kumaliza njaa na umaskini uliokithiri.
Bwana Ludovic Utouh ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania. Aidha, ameteuliwa mwaka 2012 na baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa, kwa kipindi cha miaka sita.
Wakati Baraza la Haki za Binadamu likipitisha leo tarehe 23 Julai azimio la kuunda tume ya uchugunzi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea Gaza, watoto wanaendelea kuwa wahanga wa kwanza wa mashambulizi yanayoendelea katika ukingo wa Gaza.
Kila mwaka, tarehe 18 Julai imekuwa ikiadhimishwa kama Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela, tangu siku hiyo ilipoanzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Novemba 2009, ili kuenzi mchango wa Hayati Nelson Mandela kwa kukuza demokrasia, haki kwa watu wa rangi zote na maridhiano.
Leo Julai 18 ni siku ya kimataifa ya Mandela duniani. Mandela atakumbukwa kwa sifa nyingi na mchango wake kwa dunia. Mandela amesifika katika sio tu nchi yake lakini duniani kote kwani aliyagusa maisha ya wengi.
Lengo la kwanza katika malengo ya maendeleo ya milenia ni kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa. Wakati malengo hayo yanafika ukomo mwakani, bado mtu mmoja kati ya wanane ameathirika na njaa duniani.
Uimarishaji wa afya ya uzazi ni lengo nambari tano katika malengo ya milenia ambayo yatafikia ukomo mwakani.
Wakati malengo ya maendelo ya milenia yanatarajia kufikia ukomo mwakani, Umoja wa Mataifa umezindua ripoti kuhusu mafanikio yaliyopatikana.
Nchini Afrika Kusini, mashirika ya kimataifa na wadau mbali mbali wa misaada ya kijamii na ya kibinadamu wamekutana kwa ajili ya kongamano la tatu kuhusu afya ya akina mama, watoto na watoto wachanga.