Ugonjwa wa saratani waangaziwa nchini Tanzania
Jumanne ijayo tarehe Nne Februari mwaka 2014, ni siku ya saratani duniani. Maudhui ya mwaka huu ni vunja fikra potofu kuhusu saratani. Maadhimisho haya yanakuja wakati ripoti mpya kuhusu mwelekeo wa saratani duniani ikisema ugonjwa huo unazidi kuenea nchi maskini ambako tiba ni changamoto,.