Muhogo na Samaki vyabadili maisha ya wakazi wa Tanzania
Tarehe 20 Novemba kila mwaka ni siku ya maendeleo ya viwanda barani Afrika. Siku hii iliidhinishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1989 kwa lengo la kuangazia viwanda kama moja ya sekta muhimu za kuchagiza maendeleo barani humo.