Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Picha na UN News/Yasmina Guerda

Anasemekana kuwa mwanamke wa kwanza wa kanda ya Afrika mashariki na kati kupata shahada ya Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza mwaka wa 1954.

Wakati  harakati za siku 16 za kuhamasisha kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake zikiwa zinaendelea, leo tuko nchini Uganda kusikia mchango wa mama mmoja ambae sasa ni marehemu lakini alikuwa mpigania haki za wanawake nchini humo. Dkt Sarah NYENDWOHA Ntiro ambae anasemekana kuwa mwanamke wa kwanza kanda ya Afrika mashariki na kati kupata shahada ya Chuo Kikuu kutoka Chuo Kikuu  cha Oxford nchini Uingereza mwaka wa 1954 katika somo la Historia.

Sauti
3'12"
IOM/Amanda Nero

Nuru yaonekana katika juhudi za kulinda maeneo oevu, Uganda

Ulinzi wa mazingira umekuwa ukipigiwa upatu na Umoja wa Mataifa kama moja wa juhudi za kuona dunia yetu haihatarishwi na majanga yatokanayo  na uharibifu wa mazingira. Mito ni moja wa sehemu ambazo zinasadia maisha ya viumbe wengi kama mwanadamu na mifugo kwa kupata maji ya kunywa pamoja na matumizi mengine mengi.

Lakini  baadhi ya mito imekuwa ikichafuliwa huenda  kwa kutojua.Moja wa mito hiyo ni ule wa Kanywakono wilya ya Hoima , magharibi mwa Uganda.Kwa kuelewa zaidi hali huko ungana na mwandishi wetu John Kibego alifika huko na kutuandalia Makala ifuatayo.

Sauti
3'47"
©UNHCR/O. Akindipe

Baadhi ya watu hunyimwa haki yao ya kumiliki mali

Katika mwendelezo wa kupitia ibara za tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka huu wa 2018 linatimiza miaka 70, leo inamulikwa ibara ya 17 inayozungumzia haki ya mtu kumiliki mali yeye mwenyewe au kwa ushirika na mtu mwingine au wengine. Ibara hii inazingatia ukweli kwamba baadhi ya watu wananyimwa haki hiyo kwa misingi mbalimbali ikiwemo rangi, jinsia, kabila, dini au umri. Katika basi kuangazia utekelezaji wa ibara hiyo tunajikita katika mtu kunyimwa haki hiyo kwa misingi ya kijinsia na kutufafanulia hayo ungana na Siraj Kalyango katika makala hii.

Sauti
3'17"

Jinamizi la kutosajiliwa utotoni, laandama maelfu ya watu wasio na utaifa

Ibara ya 15 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linasisitiza haki ya mtu kuwa na utaifa. Iwe ni utaifa kwa kuzaliwa au kwa kusajiliwa katika nchi nyingine. Hata hivyo kutokana na sababu mbalimbali zaidi ya watu milioni 12 hivi sasa duniani  hawana utaifa. Ukosefu wa utaifa  unapoka watoto na watu wazima haki zao za msingi. Je ni sababu gani basi zinafanya watu wakose utaifa, na ni madhila yapi basi wanapitia? Ungana basi na Grace Kaneiya katika makala hii.

Sauti
3'11"
UNIC Mexico/Antonio Nieto

Inahitaji utashi wa serikali kutekeleza ibara za haki za binadamu

Ibara ya 14 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa  inaeleza kuwa kila mtu ana haki ya kusaka na kuomba hifadhi katika nchi nyingine ikiwa anateswa nchini mwake.Katika mazungumzo na Arnold Kayanda, Mwanasheria, Wakili wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania, Jones Sendodo anasema inahitaji utashi wa serikali zilizoko madarakani kutekeleza ibara hizi kwani kuna hata nchi ambazo pamoja na kuridhia sheria na kanuni zinazowataka kutekeleza haki za binadamu, bado hazifanyi hivyo.

Sauti
3'2"
UN/Elma Okic Edit

Je wajua maana ya haki ya faragha kwa mujibu wa tamko la haki za binadamu?

Mtu ana  haki ya kuwa na faragha katika maisha yake na hii ni kwa mujibu wa ibara ya 12 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Neno faragha lina maana pana zaidi ambapo katika uchambuzi wa Ibara kwa Ibara za tamko hilo kwenye kuelekea kilele cha  miaka 70 ya tamko hilo, leo Siraj Kalyango amezungumza na mtaalamu wa sheria kutoka Tanzania ili uelewe zaidi.

Audio Duration
2'50"
UNICEF/Seck

Asante Tanzania lakini nyumbani ni nyumbani:Wakimbizi wa Burundi


Maelfu ya wakimbizi wa Burundi wanaopata hifadhi nchini Tanzania wanaendelea kurejea nchini mwao kwa msaada wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR kufutia makubaliano maalum kati ya serikali ya Burundi na ya Tanzania yaliyofikiwa yaliyoafikiwa katika mwezi Machi mwaka huu. Kufikia sasa inakisiwa wakimbizi takriban elf 72 watakuwa wamerejea Burundi kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Wakimbizi wapatao elf mbili wanaondoka kila wiki kwenye kambi tatu zilizoko magharibi mwa Tanzania na kurudi Burundi

Sauti
4'26"
UN News

Mahakama zinapaswa kuwa huru na zisiegemee upande wowote- Dkt. Laltaika

Katika mwendelezo wa uchambuzi wa tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, leo tunaangazia ibara ya 10 ambayo inasema kwamba Kila mtu mwenye kesi ana haki ya kusikilizwa kwa haki katika mahakama iliyo wazi kwa umma,yenye kujitegemea, huru na isiyo na upendeleo. Nini basi maana ya ibara hii? na je nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambazo zimeridhia tamko hili zinafuata? Kufahamu hayo na mengine mengi, Assumpta Massoi amezungumza na Dkt.

Sauti
4'8"
UNSMIL/Iason Athanasiadis

Mtu hapaswi kukamatwa kiholela

Nchi zinatakiwa kubadili sheria zao ili kwenda sawa na mbinu za sasa za utumwa na utwana.

Ibara ya 9 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linalotimiza miaka 70 mwaka huu wa 2018, inaeleza hakuna mtu anayepaswa kukamatwa kiholela na kuwekwa ndani au kulazimishwa kwenda uhamishoni. Lakini je!    Nchi wanachama zinatimiza matakwa ya ibara hii? Anold Kayanda wa idhaa hii  amezungumza na Mwanasheria, wakili Jebra Kambole wa Tanzania anaeleza.

Sauti
3'7"