Mkakati maalum wa kujenga vyoo waandaliwa India
Usafi wa vyoo nchini India bado ni changamoto kubwa. Takwimu zinaonyesha kuwa nchi hiyo ni miongoni mwa zile zinazoongoza kwa upungufu wa vyoo, lakini sasa kuna habari njema kwani mradi maalum umeandaliwa ukiwa na lengo la ujenzi wa vyoo utakaoleta nuru kwa wakazi wa India .