UNAIDS imetaka kuwepo na uhuru wa kimataifa wa kutembea kwa watu wanaishi na virusi vya HIV
Mkuu wa Bodi la Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya ukimwi (UNAIDS) Michel Sidibe, ametoa wito wa kuwepo uhuru wa kimataifa wa kutembea kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kwa mwaka huu wa 2010, mwaka ambao nchi mbalimbali zimeazimia kufikia malengo ya kimataifa ya kuzuia virusi vya ukimwi, kupata matibabu, huduma na msaada unaohitajika kwa wanaoishi na virusi hivyo.