Kuadhimisha siku ya ukimwi duniani UNICEF yazindua ripoti ya AIDS na watoto
Tarehe mosi Desemba kila mwaka huadhimishwa siku ya ukimwi duniani huku shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS, shirika la afya duniani WHO, shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF ,mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na wadau wa kupambana na ukimwi hutoa tathimini ya hatua zilizopigwa wapi palipo na mapungufu na nini kifanyike kuendelea kunusuru maisha ya watu kutokana na ugonjwa huo hatari usio na tiba hadi sasa.