Burundi imehitimisha mchakato wa uchaguzi uliosusiwa na wapinzani
Baada ya kampeni, hekaheka na upigaji kura kwa miezi miwili sasa Burundi imefunika ukurasa wa uchaguzi mkuu wiki hii.
Baada ya kampeni, hekaheka na upigaji kura kwa miezi miwili sasa Burundi imefunika ukurasa wa uchaguzi mkuu wiki hii.
Zaidi ya wanajeshi 200 wa kikosi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na kile cha muungano wa Afrika UNAMID katika jimbo la Darfur nchini Sudan hii leo wameendesha shughuli ya siku nzima ya usafi pamoja na kampeni za kuhamasisha wakaazi wa jimbo hilo kuhusisna na umihimu wa mazingira safi.
Umoja wa Mataifa umeshutumu hatua za kufukuzwa kazi kwa majaji watatu na hakimi mmoja nchini Honduras kufuatia kile kinachotajwa kuwa walitoa maoni kuhusiana na mzozo wa kiasia ulioshuhudiwa nchini humo, ukisema kuwa hatua zinawatisha wengi wa majaji katika taifa hilo la Amerika ya kati.
Ripoti ya mkutano wa Umoja wa Mataifa wa biashara na maendeleo UNCTAD iliyotolewa leo inasema uzalishaji wa chuma cha pua ulipungua sana mwaka jana lakini mahitaji ya bidhaa hiyo yamehakikisha biashara inaendelea tena.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na washirika wake leo wametangaza kuwa pembe ya Afrika kwa mara nyingine iko huru na virusi vya polio.
Eneo la Basunkusu kaskazini mwa jimbo la Equateur nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limeathirika vibaya na mafuriko.
Mvua zinazoendelea kunyesha zinauia juhudi za jumuiya ya kimataifa ya misaada kutathimini athari zilizosababishwa na mafuriko nchini Pakistan.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limesikitishwa na taarifa ya kurejeshwa nyumbani kwa nguvu wakimbizi wa Kisomali.
Watu wapatao 90,000 wamearifiwa kuzikimbia nyumba zao eneo la Ben jimbo la Kivu ya Kaskazini nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia operesheni za kijeshi baina ya serikali, wapiganaji wa kundi la FARDC na pia muungano wa jeshi la ukombozi Uganda ADF-NALU.
Wiki ya unyonyeshaji duniani hufanyika kila mwaka kuanzia Agosti mosi hadi 7 katika nchi zaidi ya 120.