Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

OCHA/ Trond Jensen

Mafuriko Nigeria yaathiri zaidi ya watu milioni 3 na kukatili maisha ya watu 600: OCHA

Mafuriko makubwa yanayoikumba Ningeria hivi sasa hayajawahi kushuhudiwa kwa zaidi ya muongo mmoja limesema Ofisi ya Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA na kuongeza kuwa hadi kufikia sasa zaidi ya watu milioni 3 wameathirika wengine wakipoteza maisha, zaidi ya milioni kutawanywa na miundombinu muhimu ikiwemo nyumba, barabara na mashamba vimesambaratishwa.

Sauti
3'53"
UN/ Flora Nducha

Rwanda imetupokea na kutukirimu: Wahamiaji toka DRC

Hali tete ya usalama inayoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC imewafanya watu wengi kufungasha virago kuyakimbia makazi yao na Kwenda kusaka usalama na mustakbali bora sehemu zingine ndani nan je ya nchi hususani nchi Jirani za Burundi, Uganda, Tanzania na Rwanda.

Sauti
7'12"
UNDP/ Sawiche Wamunza

UNDP na wadau waanza kuelimisha wanawake na vijana yaliyomo kwenye mkataba wa eneo huru la biashara Afrika, AfCFTA

Mwaka 2018 nchi za Afrika zilitia saini makubaliano ya kuwa na eneo la biashara huru, AcFTA makubaliano ambayo yalianza kutekeleza mwaka 2019 na kulifanya kuwa eneo kubwa zaidi la eneo huru la biashara duniani likiwa na nchi 54 na jumla ya watu bilioni 1.2. Mwezi Septemba mwaka huu wa 2022 nchini Tanzania kulifanyika kongamano la siku 3 la wanawake na vijana wafanyabiashara chini ya mwamvuli wa AcFTA likifunguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania ambaye ndiye mlezi wa jukwaa la wanawake na vijana AcFTA.

Sauti
5'52"
UNMISS

UNMISS yawajengea uwezo wafanyabiashara nchini Sudan Kusini

Ushirikiano na ukuaji kiuchumi ni miongoni mwa masuala muhimu katika kuhakikisha nchi yoyote ina amani na wananchi wake wanapata Maendeleo. Na ili kuhakikisha wananchi wa Sudan Kusini wana amani na maendeleo, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda Amani nchini humo UNMISS umeandaa warsha ya biashara lengo likiwa ni kuwatia moyo wafanyabiashara wa ndani na kuwawezesha kiuchumi ili nao waweze kuimarisha biashara zao lakini pia waweze kufanya biashara na Umoja wa Mataifa .

Sauti
3'34"
UNCDF Tanzania

UNCDF yawanufaisha wakulima wa viazi lishe Mkoani SIMUYU

Tarehe 24 Oktoba dunia ilisherehekea siku ya Umoja wa Mataifa kwa kuadhimishwa miaka 77 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1945. Ingawa kuanzishwa kwake kuliangalia zaidi masuala ya Amani na usalama na Haki za Binadamu lakini Shirika hili kubwa la kimataifa limezidi kupanua wigo wake na sasa wanashiriki katika sekta zote duniani, lengo likiwa ni kuboresha maisha ya watu wote na kuhakikisha wana ustawi wa maisha na pale kwenye changamoto shirika husika la Umoja wa Mataifa hutafuta ufumbuzi.

Sauti
6'5"
Benki ya Dunia/ Screenshot

Mashirika yasiyo ya kiserikali Tanzania yachukua hatua kukabili madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa watoto

Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kubainishwa kila uchao. Mathalani hivi karibuni ripoti ya mashirika ya Umoja wa Matiafa ilitaja kuwa watoto milioni 559 kwa sasa wanakabiliwa na joto Kali na hali inategemewa kuwa mbaya zaidi ambapo mpaka kufikia mwaka 2050 watoto wote duniani ambao wanakadiriwa kuwa bilioni 2.02 watakumbwa na madhara ya joto kali. Joto kali ni moja ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi.

Sauti
4'11"
UNICEF Zambia

Mradi wa UN Zambia warejesha watoto wa kike shuleni, wazazi wafurahia

Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake lile la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA na la kuhudumia watoto, UNICEF  huko nchini Zambia unatekeleza mradi wa kuchochea kasi ya kutokomeza ndoa za utotoni, GPECM. Mradi unalenga kulinda na kuendeleza watoto wa kike na barubaru ili kuzuia mimba na ndoa za utotoni na hatimaye wafikie malengo ya juu ya ustawi kielimu, kiuchumi na kijamii.

Sauti
4'23"