Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makala

Watu Asili kushiriki na kushirikishwa katika utunzaji wa mazingira na viumbe hai: Burundi

Kongamano la watu asili kutoka  eneo la Maziwa makuu  barani Afrika limehitimishwa mjini  Bujumbura Burundi . Lilijikita katika jinsi Jamii hiyo wanavyoweza kushiriki na  kushirikishwa katika utunzaji wa mazingira na viumbe hai katika maeneo wanakoishi.

Jamii hiyo imekuwa inanyooshewa kidole kwa kuhusika na sehemu kubwa katika uharibifu wa mazingira, madai ambayo wanayakana wakitaja kwamba mazingira ni sehemu ya maisha yao.

Sauti
4'4"
UN/Comoro

Tozo za ushuru ziangaliwe upya ili kukuza uchumi- Bakhresa

Lengo namba 8 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs linasisitiza ukuaji wa uchumi tena ulio jumuishi. Nchi za Afrika zilizo mashariki mwa bara hilo zinaelezwa kuwa ziko mstari wa mbele kuhakikisha uchumi unakua ili hatimaye kukuza vipato vya wanachi na hivyo kuondoa umaskini.

Hivi karibuni katika mkutano uliofanyika huko Comoro na kuandaliwa na tume ya uchumi barani Afrika, ECA, washiriki kutoka sekta ya umma na binafsi walipazia sauti fursa na changamoto katika ukuaji wa uchumi. Shuhuda wetu alikuwa Priscilla Lecomte kutoka ofisi ya ECA, mjini Kigali nchini Rwanda.

Sauti
6'25"

Kazi ni kazi , ukiitilia maanani:

Shirika la la kazi   duniani ILO, linesema ukosefu  wa  ajira kwa vijana bado ni changamoto kubwa  duniani kote.   Umoja wa Mataifa  na mashirika yake wamekuwa mstari wa mbele kuhimiza serikali na asasi za kiraia kutoa mafunzo yatakayowezesha vijana kujiajiri ili kuepuka zahma ya kutokuwa na ajira.

Katika taaluma za kiufundi moja ya mbinu ya kuzifunza kazi kwa baadhi ya vijana ni kupata fursa ya kijifunza taaluma kupitia kwa wazazi wao. Vijana wengi wamejikuta wamerithi kazi za babu, baba zao, mama au ndani ya familia.

Audio Duration
4'8"

Wengine wataka kutumia matambara kujisitiri hedhi

Suala la wanawake na wasichana kujisitiri wakati wa hedhi limesalia kuwa kizungumkuti hasa katika nchi maskini zijulikanazo pia kama nchi zinazoendelea. Hii ni kutokana na kwamba katika jamii nyingi za maeneo hayo suala hilo ni mwiko kuzungumzwa  hadharani na pia  pedi za kisasa ambazo hazina madhara ya kiafya ni vigumu kuzimudu kwa kuwa ni ghali. Hii inawalazimu baadhi ya wazazi kuwashauri watoto wao kutumia nguo kuukuu kujisitiri kama njia mbadala. Lakini hilo madaktari wanasema halifai. Kupambanua mvutano huo Siraj Kalyango anakualiaka kwenye Makala hii.

Sauti
3'59"

Wachuuzi wa samaki Burundi na mafunzo ya kuepusha uchafuzi wa mazingira

Ziwa  Tanganyika kwenye ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika, limekuwa mashuhuri sio kwa kusafirisha watu na bidhaa bali pia katika kuzalisha  samaki  aina mbalimbali  Lakini changamoto kubwa ni uhifadhi za samaki  baada ya kuvuliwa hadi kuliwa ili kuepusha uchafuzi wa mazingira. Ingawa samaki huonekana  kwa wengi kama chakula bora, lakini kama hawatahifadhiwa vyema wanaweza kusababisha madhara makubwa  kwa watumiaji na mazingira.

Sauti
4'17"
UNHCR/Caroline Bach

Muziki ni daraja la ushirikiano kwa watoto wakimbizi

Sanaa ya Muziki hutumika kama chombo cha ushirikiano wa kijamii na imeleta nuru kwa watoto na vijana wakimbizi wanaosaka hifadhi nchini Sweden.  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR kwa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la El Sistema wameandaa tamasha la muziki huko Stockholm linaloleta pamoja wakimbizi kutoka Syria, Afghanistan, Eritrea, Albania, Venezuela na wenyeji wa Sweden.

Audio Duration
3'52"

Kutoa ni moyo wala si utajiri

Kutana na mama Shamsa Abdilahi, yeyé na mumewe walikuwa wakimbizi kutoka Somalia ambao wameishi Uingereza kwa miaka kadhaa. Ametambua umuhimu wa kusaidia alipokuwa na mahitaji, na akaahidi kurejea nyumbani mambo yatakapokaa sawa ili kurejesha hisani.

Sauti
4'21"
UN News/Patrick Newman

Nachukizwa sana na wanaoona wenye shida ni ombaomba- Brenda

Kwa siku nne kuanzia tarehe 8 Februari 2018 vijana kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa walikutana jijini New York, Marekani kwa ajili ya mjadala wa mustakhbali wa dunia. Mjadala huo wa vijana umefanyika kwa kuzingatia mfumo wa Umoja wa Mataifa, ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuwandaa vijana kubeba jukumu la kusongesha maendeleo kwenye nchi zao na dunia kwa ujumla. Miongoni mwao ni Brenda Kimwatan, mwanafunzi kutoka Kenya ambaye anasoma Chuo Kikuu cha Cape Town nchini Afrika Kusini.

Sauti
4'10"

Mkimbizi anatafuta maisha - JJ Bola

Umoja wa Mataifa unaendelea kusisitiza kuwa mtazamo potofu kuhusu uhamiaji na wahamiaji umeendelea kukwamisha matumizi bora ya dhana hiyo kote ulimwenguni. Umoja huo unahimiza serikali zote kuenzi mbinu tofouti za kufanya uhamiaji uwe na manufaa kwa wote, maana wakimbizi wanaweza kuchangia katika uchumi ya nchi wanamoishi. Licha ya wito huo bado wakimbizi wengi bado wanapitia machungu wanapokuwa ukimbizini, kitu ambacho kinasababisha wengi kuwaza walikotoka na machungu walioyapitia.

Sauti
3'55"

Viwanda vidogovidogo vyalaumiwa kuchafua vyanzo vya maji

Maji safi na salama ni uhai wa viumbe vyote ulimwenguni ikijumuisha binadamu, wanyama na mimea. Lengo namba 6 la  malengo ya maendeleo  endelevu, SGD linazungumzia maji safi na salama kwa kila mtu ifikapo  ya mwaka 2030.

Katika migogoro ya kimazingira, viwanda vidogo na vikubwa vimekuwa vikilalamikiwa kuharibu mazingira kwa kujenga mifereji inayopeleka maji taka katika vyanzo vya maji au mito.

Sauti
3'55"