WHO inaonya kwamba njaa inaongezeka Gaza hakuna chakula wala nishati ya kupikia na kukaribisha magonjwa zaidi
Njaa imeukumba Ukanda wa Gaza kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na hivyo kutishia ongezeko la magonjwa hususan miongoni mwa watoto, kina mama wajawazito na wanaonyonyesha na makundi mengine yaliyo hatarini na nishati ya kupikia nayo imeota mbawa.
Jifunze Kiswahili: Tofouti ya matumizi ya "Habari kwa ufupi na Muhtasari wa habari"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua tofauti ya maneno “HABARI KWA UFUPI NA MUHTASARI WA HABARI”
UN: Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa Binadamu ni kusherehekea Umoja wetu katika tofauti zetu
DAFI, Mfuko wa Ufadhili wa Kimasomo kwa Wakimbizi, kwa kushirikiana na UNHCR wanawasaidia wakimbizi kutimiza ndoto zao za kupata elimu ya juu katika nchi ya kwanza wanakopata hifadhi baada ya kuzikimbia nchi zao.
UNICEF Tanzania: Chanjo ya polio sio tu inamlinda mtoto bali inaokoa maisha
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linahimiza kila nchi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 5 wanapatiwa chanjo dhidi ya polio ugonjwa ambao sio tu unasababisha ulemavu kwa watoto lakini pia ukakatili maisha yao.
Uchaguzi mkuu mwaka 2023 nchini DRC wafanyika kama ilivopangwa
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, uchaguzi mkuu wa Rais, Magavana, wabunge na madiwani umefanyika hii leo kama ilivyopangwa licha ya changamoto zilizojitokeza katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Wanazuoni waanza utafiti wa kupunguza maneno ya kigeni katika lugha ya kiswahili
Wakati wadau wa lugha ya kiswahili wakikuna vichwa namna ya kuhakikisha lugha hiyo adhimu inasambaa na kuzungumzwa duniani kote, wengine wanaendelea na utafiti kuhakikisha lugha hiyo inakuwa na maneno ya kiswahili fasaha na kupunguza mchanganyiko wa maneno ya kigeni katika lugha hiyo.