Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 DESEMBA 2023

19 DESEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo kesho nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ni uchaguzi mkuu ikiwa ni tamati ya kampeni huku Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umeshiriki kwa kusafirisha sio tu vifaa vya uchaguzi lakini pia kuelimisha wananchi jinsi ya kukabili na kuzia habari potofu na za uongo kwani ni tisho la amani na usalama. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani.

  1. Leo Umoja wa Mataifa umeonya kwamba Gaza ni mahali hatari zaidi kuishi kwa watoto. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, James Elder amesema, “Siku baada ya siku ukatili wa hali ya juu unadhihirika. Katika saa 48 zilizopita hospitali kubwa Zaidi iliyobaki inafanyakazi imeshambuliwa mara mbili...
  2. Nchini Sudan shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limesema linatiwa wasiwasi kubwa na kiwango cha janga la watu wanaoendelea kulazimika kutawanywa ndani ya Sudan na katika nchi Jirani.
  3. Na ripoti mpya "Hali ya mifumo ya chakula duniani kote katika kuelekea mwaka  2030", iliyochapishwa leo na mradi wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO unaoangia mifumo hiyo kuelekea ukomo wa malengo ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030 (FSCI), inatoa tathimini ya kwanza ya ufuatiliaji wa kisayansi ili kuwaongoza watoa maamuzi wanapotaka kufanya mabadiliko ya jumla ya kilimo cha kimataifa na mifumo ya chakula. 
  4. Mashinani tunakupeleka nchini Somalia kusikia ujumbe kuhusu uwezo wa filamu katika simulizi ya hadithi za utamaduni na haki za binadamu.  

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'15"