Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 DESEMBA 2023

21 DESEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo mwezi Agosti mwaka huu wa 2023, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kutangaza tarehe 21 mwezi Desemba kila mwaka kuwa siku ya mpira wa kikapu duniani. Hii ni kwa kutambua nafasi ya mchezo huu katika kuleta amani, maendeleo na ustawi wa jamii. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na ufafanuzi wa tofouti ya maneno. 

  1. Mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yameendelea kusisitiza wito wa usitishwaji mapigano Gaza kwani hali inazidi kuwa mbaya kila uchao, lile la afya duniani WHO limesema timu yake ilifanikiwa kufika katika hospitali za Al Ahil Arab na Al Shifa Gaza kaskasini na uharibifu walioushuhudia hauelezeki. Dkt. Richard Peeperkorn akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo amesema “Wafanyikazi wetu wanakosa maneno ya kuelezea hali mbaya zaidi inayowakabili wagonjwa na wahudumu wa afya waliobaki katika hospitali hizo..
  2. Takriban watu 300,000 wamefungasha virago na kukimbia katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Sudan wa Wad Madani kwenye jimbo la Aj Jazirah kwa mujibu wa shirika la umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM kufuatia wimbi jipya la mapigano ambayo pia yametawanya maelfu ya watu ndani ya jimbo hilo.
  3. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC hapo jana watu wapatao milioni 44 walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na wawakilishi wa serikali za mitaa. Rais wa tume ya uchaguzi nchini humo CENI Denis Kadima amesema wale wote walioshindwa kupiga kura jana kwa sababu mbalimbali ikiwemo mvua leo wamepiga kura zao na matokeo ya awali yameanza kubandikwa katika baadhi ya vituo huku zoezi la kuhesabu kura likiendelea nchi nzima.. 
  4. Katika kujifunza Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua tofauti ya maneno. 

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
10'59"