Ukataji wa miti watishia uoto wa asili DRC
Wakati malengo ya maendeleo ya milenia yakifikia ukomo mwaka 2015, lengo namba saba ambalo ni utunzaji wa mazingira linakumbana na changamoto nyingi ikiwamo ukataji hovyo wa miti.
Wakati malengo ya maendeleo ya milenia yakifikia ukomo mwaka 2015, lengo namba saba ambalo ni utunzaji wa mazingira linakumbana na changamoto nyingi ikiwamo ukataji hovyo wa miti.
Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC mizozo na mapigano Mashariki mwa nchi hiyo vimesababisha siyo tu kupotea kwa maisha ya watu bali pia machungu kwa wale wanaobakia.
Wahenga walisema elimu haina mwisho na hivyo fursa yoyote ya kujifunza inapojitokeza ni vyema kuitumia ipasavyo kwani inaweza kubadili maisha siyo ya anayejifunza tu bali pia ya jamii yake.
Siku ya Ijumaa tarehe Tano Disemba mwaka 2014, mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC huko The Hague, Uholanzi ilitupilia mbali mashtaka dhidi ya Uhuru Kenyatta.
Tarehe 5 Mwezi Disemba kila mwaka ni siku ya kimataifa ya kujitolea siku ambayo hutumiwa na jumuiya ya kimataifa kuhamasisha kujitolea kwa maendeleo ya jamii.
Unyanyapaa ni tatizo kubwa kwa vijana wanaoambukizwa virusi vya Ukimwi, amesema Grace Muthoni, kiongozi wa taasisi iitwayo Max Facta Youth Group inayojishughulisha na vijana waliopata maambukizi ya ukimwi nchini Kenya.
Wakati mkutano wa 20 wa nchi wanachama kuhusu masuala ya mazingira, COP20 unaendelea huko Lima, Peru wawakilishi wa nchi mbali mbali wamekutana kushiriki katika majadiliano ya kuwezesha kufikiwa kwa mkataba wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi baadaye mwakani huko Paris, Ufaransa.
Wakati siku ya ukimwi duniani imeadhimishwa leo Disemba mosi huhu kukitajwa baadhi ya mafanikio yaliyopatikana hadi sasa, bado kuna changamoto kadhaa ambazo zinakwamisha lengo la kutokomeza kabisa ukimwi . Mathalani upatikanaji wa huduma na tiba kwa wale wanaoishi na virusi vya Ukimwi.
Tarehe 20 Novemba kila mwaka ni siku ya maendeleo ya viwanda barani Afrika. Siku hii iliidhinishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1989 kwa lengo la kuangazia viwanda kama moja ya sekta muhimu za kuchagiza maendeleo barani humo.
Mwanamke mmoja kati ya watatu duniani kote amekumbwa na ukatili wa kijinsia! Ukatili huo ni pamoja na kupigwa, kubakwa na hata kunajisiwa wakati akiwa utotoni.