Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi Kamau azungumzia uamuzi wa ICC kuhusu Kenyatta

Balozi Kamau azungumzia uamuzi wa ICC kuhusu Kenyatta

Pakua

Siku ya Ijumaa tarehe Tano Disemba mwaka 2014, mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC huko The Hague, Uholanzi ilitupilia mbali mashtaka dhidi ya Uhuru Kenyatta. Mwendesha Mashtaka Mkuu Fatou Bensouda alieleza kuwa uamuzi huo unazingatia kuwa hawana ushahidi wa kutosha wa kuweza kuthibisha pasipo shaka mashtaka matano yaliyokuwa yanamkabili Kenyatta. Kufuatia uamuzi huo, Joseph Msami wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa, alizungumza na Mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Macharia Kamau ambaye hapa anaanza kwa kuelezea walivyopokea tangazo hilo.

Photo Credit
Mwakilishi wa kudumu wa Kenya katika Umoja wa Mataifa Balozi Macharia Kamau.(Picha ya UM/Mark Garten)