Ziara ya Mkuu wa MINUSCA huko Boyo yabaini mahitaji ya wananchi
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Denise Brown ametembelea eneo ambalo mwezi uliopita lilikuwa lilishambuliwa na watu wenye silaha na kusababisha vifo vya makumi kadhaa ya watu huku wengine wakikimbia makazi yao.