Baraza la Usalama ungeni mkono kwa dhati hatua za kutokomeza M23- Bi. Pobee
Ongezeko la hivi karibuni la mashambulizi kutoka kikundi cha waasi cha M23 huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC linatishia amani, usalama na utulivu kwenye ukanda mzima wa Maziwa Makuu barani Afrika na hivyo hatua za dharura za kudhibiti ghasia hizo zinahitajika, amesema Afisa Mwandamizi wa Umoja wa Mataifa hii leo wakati akihutubia Baraza la Usalama la umoja huo jijini New York, Marekani.