Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mkimbizi Cavine Abalo mwenye umri wa miaka 20 akiwa na mwanae mwenye umri wa miezi mitatu katika wilaya ya Lamwo nchini Uganda.
UNICEF/Jimmy Adriko

Dola milioni 47.8 zahitajika haraka kukidhi mahitaji ya wakimbizi Uganda:UNHCR 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wengine 44 wa misaada ya kibinadamu wametoa ombi la dharura la dola za Marekani milioni 47.8 ili kukabiliana na mahitaji muhimu ya maelfu ya wakimbizi waliofika Uganda mwaka huu, wakikimbia ghasia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na za mapigano ya hapa na pale nchini Sudan Kusini.  

Sekta ya maziwa ya watoto ya viwandani hutumia mabilioni ya fedha kila mwaka kushawishi uamuzi wa wazazi juu ya kile ambacho watamlisha mtoto wao
WHO/UNICEF

Kampuni za maziwa ya watoto zatumia mitandao ya kijamii kurubuni wazazi

Kampuni zinazotengeneza maziwa ya watoto ya unga zinalipa majukwaa ya mitandao ya kijamii na watu wenye ushawiwishi ili kuweza kuwafikia wajawazito na akina mama kama mbinu mojawapo ya kuuza bidhaa zao, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO hii leo, likiongeza kuwa harakati hizo zinafikisha ujumbe kwa wanawake wao katika kipindi chenye changamoto zaidi kwenye maisha yao.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine
UN /Eskinder Debebe

Guterres awaambia waukraine 'dunia inawaona' huku akiahidi msaada zaidi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameielezea Ukraine kama "kitovu cha maumivu na zahma isiyovumilika", alipozungumza na wanahabari leo mjini Kyiv akiwa pamoja na mwenyeji wake rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine na kuahidi kuongeza msaada kwa watu wa taifa hilo huku kukiwa na mateso makubwa , na mamilioni ya watu wamekimbia makazi yao kutokana na uvamizi wa Urusi. 

Christian Ngwe, kiranja katika shule ya msingi ya Nganda Yala jijini Kinshasa nchini DRC, akiwa amepiga picha mbele ya jengo la vyoo vipya vya shule yao.
© UNICEF/Jean-Claude Wenga

UNICEF DRC yawezesha wanafunzi kujivunia shule yao 

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa msaada kutoka eneo la mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, limeimarisha huduma za usafi na kujisafi WASH, kwenye shule moja mjini Kinshasa na hivyo kuwezesha wanafunzi kujifunza katika mazingira safi na salama.

Sauti
1'51"