Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mpaka wa Burundi na DR Congo. UNHCR inawasaidia wakimbizi wa Burundi waliokuwa DR Congo kurejea nyumbani.
Screenshot

Waliokuwa wakimbizi nchini DRC wafurahia kurejea nyumbani Burundi  

Raia 272 kutoka familia 78 wa Burundi waliorejea nchini Burundi kutoka kambi ya wakimbizi ya Lusenda katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwishoni mwa wiki iliyopita wamekaribishwa na wanachi wenzao, serikali na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi ili waanze maisha katika nchi yao waliyoikimbia kwa vipindi tofauti kutokana na hali mbaya ya usalama 

Wasichana wadogo katika kambi ya wakimbizi wa ndani nchini Myanmar wanachota maji kutoka kwenye kisima.
UNOCHA/Z. Nurmukhambetova

Nasimama katika mshikamano na watu wa Myamnar : Guterres

Ikiwa hapo kesho Jumanne, Februari 1,2022 ni maadhimisho ya mwaka mmoja tangu jeshi la Myanmar kupindua Serikali ya kiraia iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia na kuwaweka kizuizini kiholela viongozi wa Serikali, akiwemo Mshauri wa Serikali Aung San Suu Kyi na Rais Win Myint. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema anasimama katika mshikamano na watu wa Myanmar na matarajio yao ya kidemokrasia kwa jamii jumuishi na ulinzi wa jamii zote, ikiwa ni pamoja na Rohingya.

Mama na binti yake huko Barranquilla, Colombia. Mamlaka za kitaifa zinakwenda nyumba kwa nyumba ili kudhibiti mbu wanaoweza kubeba Zika, Dengue na Chikungunya. PAHO/WHO Joshua E. Cogan
PAHO/WHO Joshua E. Cogan

Juhudi za pamoja zinahitajika kukomesha Magonjwa ya Kitropiki yasiyopewa Kipaumbele:WHO

Katika maadhimisho ya Siku ya Magonjwa ya Kitropiki yasiyopewa kipaumbele Duniani Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limetoa wito kwa kila mtu, kujiunga pamoja ili kukabiliana na ukosefu wa usawa unaojitokeza katika magonjwa yasiyo ya kuambukiza na kuhakikisha jamii maskini zaidi na zilizotengwa ambazo zimeathiriwa zaidi na magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika zinapata huduma za afya wanazohitaji.