Camara Mariama Ciré: Mfano wa kuigwa kupitia kwenye kilimo Guinea Conakry
“Habari, naitwa Camara Mariama Ciré kutoka Guinea Conakry…,” ndivyo anavyoanza Mariama Camara Cire kwa kujitambulisha kuwa anatokea Guinea Conakry moja ya nchi za Afrika Magharibi inayopakana na Bahari ya Atlantiki katika upande wake wa Magharibi na kwingine ikipakana na Guinea Bissau, Sierra Leone, Côte d'Ivoire, Senegal na Mali.